Last Updated on 14/10/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Mimba huanza kuonekana baada ya siku ngapi
Haya ni maswali ninayoulizwa mara kwa mara;
- Dalili za kupata mimba ni zipi
- Muda gani mimba inajulikana
- Mimba inaonekana muda gani
- Mimba hupimwa muda gani
- Mimba huanza kuonekana muda gani
- Mimba hugundulika baada ya siku ngapi
- Mimba hujulikana baada ya siku ngapi
- Mimba inajulikana baada ya muda gani
- Mimba inaonekana siku ngapi
- Je mimba inaonekana baada ya siku ngapi
- Je mimba huonekana baada ya siku ngapi
- Mimba huanza kuonekana baada ya siku ngapi
- Mimba huonekana kwenye kipimo baada ya muda gani
- Mimba hujulikana baada ya siku ngapi
- Tumbo la mimba huonekana miezi mingapi
- Mimba inaanza kuhesabiwa lini
Soma hii pia > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka
Vipimo vya ujauzito vinaweza kutoa majibu ikiwa una ujauzito au la baada ya siku ya kwanza ya kukosa siku zako. Hata hivyo kuna baadhi ya vipimo vinaweza kutoa majibu ya kuwepo kwa mimba hata siku 4 au 5 kabla ya kuanza siku zako.
Kama una mzunguko ambao ni sawa yaani mzunguko mzuri ambao haubadiliki badiliki inaweza kuwa rahisi kwako kujua ni lini utaanza kuona siku zako.
Kama mzunguko wako haueleweki inashauriwa usubiri wiki 2 mpaka 3 ndiyo upime kuona kama umepata ujauzito au la kulingana na dalili utakazokuwa unaziona.
Mara nyingi ukipima ukapata majibu ya ndiyo unao ujauzito (positive) hilo huwa ndiyo jibu la kweli zaidi kuliko kama ukiambiwa hauna mimba (negative).
Hivyo wakati mwingine kuna uwezekano kipimo kikasema huna mimba lakini kumbe tayari unayo!
Ikiwa unahisi ni mjamzito halafu bado kipimo kinasema hauna nakushauri usubiri siku 7 hivi na upime tena.
Ikiwa hata baada ya kupima mara 2 au 3 na bado unapata majibu ya kuwa huna ujauzito ni vema ukafika hospitali na ufanye vipimo kwa vipimo vikubwa zaidi ikiwemo kipimo cha ‘Ultrasound‘ na ikiwa bado inaonekana huna ujauzito basi kuna uwezekano mkubwa homoni zako zikawa hazipo sawa.
Je lini hasa naweza kuwa nilipata ujauzito?
Vipimo vya ujauzito huangalia uwepo wa homoni ya mimba ijulikanayo kwa kitaalamu kama ‘Human Chorionic Gonadotrophin (HCG)’, kwenye mkojo wako.
Mwili wako huanza kuizalisha homoni hii mara tu baada ya kuwa umepata ujauzito.
Ikiwa utafanya kipimo siku moja baada ya siku uliyokosa kuona siku zako na ukapata majibu ya kuwa ni mjamzito kuna uwezekano ukawa tayari na ujauzito wa wiki mbili hivi.
Vipimo vikubwa zaidi vya ujauzito vinaweza kutoa majibu ya uhakika ikiwa ni mjamzito kuanzia siku ya 8 hivi tangu mimba ilipotungwa.
Baadhi ya vipimo vinaweza hata kukupa makadirio juu ya lini hasa unaweza kuwa ndiyo hasa ulipata ujauzito kutegemea na usawa wa homoni ya mimba kwenye mkojo wako.
Mimba huanza kuhesabiwa tangu siku ya kwanza ilipotungwa.
Dalili za kupata mimba ni zipi
Dalili za Mimba Changa
Dalili na ishara zingine za mwanzo za mimba ni pamoja na:
- Mabadiliko ya kihisia
- Kukojoa mara kwa mara
- Kuumwa kichwa
- Maumivu ya mgongo eneo la chini
- Matiti kuuma
- Chuchu kuwa nyeusi
- Uchovu
- Homa za asubuhi
Soma hii pia > Dalili 33 za mimba
Kama unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito bonyeza hapa.
Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine.
Mimba ya siku4 inaweza kuonekana ikipimwa ?
Siku ya kubeba mimba
Ninashida ya kujua no siku ya ngapi mimba uanza kutungwa baada ya tendo la ndoa
Nimepima lkn kipimo kinasema Sina ujauzito lkn kichwa kinauma nachoka Sana mgongo nao unauma vilevile maziwa pia yanaumaa
Pole sana ndugu
habar za majukum samahan mimi najihis dalili zote za kua mjamzito kichwa kinaniuma mno uchovu, homa, mate kujaa mdomon na matone ya dam yabatoka ila tangu niingie siku za hatar na ndo nlizokutana na mume wangu ni siku kumi tu je apo nikipima mimba naweza kuiona au ad zifike wiki mbili kuendelea
Mimba ya wiki moja inaweza kuonekana kwenye kipimo