Last Updated on 17/07/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Siku za kuwa mwezini kwa kawaida kwa mwanamke huwa ni kati ya siku 3 mpaka 7.
Hata hivyo hutokea kwa baadhi ya wanawake hasa wale wenye umri mkubwa wanapata hedhi kwa siku nyingi zaidi ya siku 7 na huambatana na kupata damu nzito na yenye mabonge mabonge sambamba na maumivu makali.
Tatizo hili kitaalamu hujulikana kama ‘Menorrhagia’, na ni tatizo ambalo mara nyingi hutokana na homoni kutokuwa sawa, uvimbe kwenye kizazi, maambukizi kwenye kizazi, matumizi ya baadhi ya dawa za uzazi wa mpango nk
Ikiwa unahitaji kufahamu namna ya kutibu tatizo hili la hedhi isiyoisha basi endelea kusoma makala hii kwani ina jibu la tatizo lako.
Nini husababisha kupata hedhi isiyoisha?
Sababu ya kupata hedhi isiyoisha au inayojirudia mara 2 au 3 ndani ya mwezi hutofautiana toka mwanamke mmoja hadi mwingine.
Ikiwa unatokewa na tatizo hili ni mhimu kuonana na daktari mapema kwa uchunguzi na msaada zaidi.
Sababu za tatizo hili ni pamoja na hizi zifuatazo:
1. Homoni kutokuwa sawa
2. Uvimbe kwenye kizazi
3. Ujauzito kutoka
4. Mimba kutunga nje ya kizazi
5. Baadhi ya saratani (saratani ya shingo ya kizazi)
6. Matatizo kwenye mirija ya mayai ya uzazi
Wanawake hujisikia vibaya au kuumwa kabisa wakati wakiwa kwenye siku zao sababu ya kiasi kingi cha usawa wa homoni ya estrogen na homoni kutokuwa sawa.
Pendelea vyakula vifuatavyo ili kurahisisha matibabu yako:
1. Kula zaidi vyakula vyenye madini ya chuma
Madini ya chuma ni viinilishe mhimu mwili unavihitaji. Kutokwa na damu nyingi au isiyoisha wakati wa hedhi hupelekea kupungua kwa madini ya chuma mwilini na kukusababishia damu kupungua mwilini
Kula zaidi spinachi, karoti, maharage, samaki wa baharini, zabibu kavu, brokoli nk
2. Kula zaidi vyakula vyenye madini ya Magnesium
Kula zaidi ndizi, mtindi na unga wa mbegu za maboga. Kumbuka kuzidisha sana vyakula vyenye madini ya magnesium huleta tatizo la kuharisha hivyo usizidishe.
3. Kula zaidi vyakula vyenye Omega-3
Wanawake wanaopata tatizo la hedhi isiyoishawanapaswa kuongeza ulaji wa vyakula vyenye omega 3.
Omega 3 huhamasisha uzalishwaji wa homoni zenye umhimu na faida zaidi mwilini
Uongezekaji wa uzalishwaji wa homoni mbaya (bad prostaglandings) huchangia kiasi kikubwa kupata hedhi yenye damu nyingi na isiyoisha
Uongezekaji wa uzalishwaji wa homoni nzuri hupunguza damu kuganda kusiko kwa kawaida na kuondoa tatizo la damu ya hedhi isiyoisha.
Omega 3 hupatikana kwa wingi kwenye samaki wa baharini, nazi, mayai, mbegu za maboga nk
4. Kula zaidi papai
Papai lina kimeng’enya kijulikanacho kama ‘papain’ amabacho huidhibiti homoni ya progesterone ambayo hutumika kuandaa mji wa uzazi kwa ajili ya kushika na kuutunza ujauzito.
Kula papai kila siku kunasaidia kulainisha misuli ya tumbo na kuweka sawa kukazika na kutanuka kwa mji wa uzazi jambo ambalo hudhibiti utokaji wa damu ukiwa kwenye siku zako.
5. Kunywa chai ifuatayo kila siku asubuhi
Tumia chai iliyoandaliwa kutokana na kijiko kidogo kimoja kimoja cha unga cha dawa zifuatazo; tangawizi, unga wa majani ya mlonge, mdalasini na kotimiri (parsley) bila kuongeza majani ya chai na utumie asali badala ya sukari kwenye chai hii kwa matokeo mazuri zaidi.
Muunganiko wa chai hii huufanya mwili kuwa na joto na hivyo kupunguza maumivu wakati wa siku zako, kusaidia kukata damu isiyoisha, kuongeza kinga ya mwili na kuweka sawa homoni.
Mambo mengine mhimu ya kuzingatia ili kupona tatizo hili:
• Pata muda wa kutosha wa kupumzika
• Kula vyakula vyenye afya na vya asili zaidi
• Usitumia chai ya rangi, kahawa na soda yoyote au kinywaji kingine chochote chenye kaffeina
• Punguza kidogo chumvi kwenye chakula
• Usitumie vidonge au dawa yoyote ya hospitali ya kuondoa maumivu
• Onana na daktari mara tu upatapo tatizo hili kwa uchunguzi na msaada zaidi
Ikiwa utahitaji Dawa ya asili ya hedhi isiyoisha bonyeza hapa.
Share post hii na jamaa zako wengine uwapendao