Dawa ya uvimbe kwenye kizazi

Dawa asili ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi

Last Updated on 17/07/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Dawa ya uvimbe kwenye kizazi

Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid.

Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.

Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.

Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.

Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.

Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.

Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;

1. Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini
2. Ujauzito
3. Uzito na unene kupita kiasi
4. Jenetiki zisizo za kawaida
5. Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu
6. Sababu za kurithi
7. Lishe isiyo sawa
8. Sumu na taka mbalimbali nk

Dalili zitakazokuonyesha una uvimbe kwenye kizazi ni pamoja na;

Dalili za uvimbe kwenye kizazi:

1. Kupata damu nyingi wakati wa hedhi
2. Maumivu makala wakati wa siku za hedhi
3. Kuvimba miguu
4. Unaweza kuhisi una ujauzito
5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Kuhisi kuvimbiwa
7. Kupata haja ndogo kwa taabu
8. Kutokwa na uchafu ukeni
9. Kupata choo kigumu au kufunga choo
10. Maumivu nyuma ya mgongo
11. Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto
12. Upungufu wa damu
13. Maumivu ya kichwa
14. Uzazi wa shida
15. Kutopata ujauzito
16. Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo
17. Maumivu ya nyonga
18. Mimba kutoka mara kwa mara (miscarriage)

Aina za Uvimbe kwenye kizazi

Kuna aina kuu nne za Fibroids

1. Intramural: Hutokea kwenye kuta za mji wa mimba (uterus). Wanawake wengi hupatwa na aina hii ya uvimbe.

2. Subserosal fibroids: Hii hukua nje ya kuta za mji wa mimba na hukua na kuwa kubwa sana.

3. Submucosal fibroids: Hutokea kwenye misuli chini ya ngozi laini ya kuta za mji wa uzazi.

4. Cervical fibroids: Hii hujenga kwenye shingo ya tumbo la uzazi (Cervix). 

Ikiwa mwanamke hapati shida ya namna yo yote katika shughuli zake za kila siku, anaweza asihitaji tiba ya aina yo yote hata kama imegundulika kuwa ana uvimbe wa fibroid.

Hii ni kutokana na ukweli kuwa mwanamke anapokaribia kukoma hedhi Uvimbe huu hunyauka wenyewe na mara nyingine kutoweka kabisa.

Ikitokea kwamba tiba imekuwa ni ya lazima, anaweza kupewa dawa au kufanyiwa upasuaji kutokana na hali ilivyo.

Ikiwa unahitaji dawa ya asili ya kuondoa uvimbe kwenye kizazi bonyeza hapa.

Imesomwa na watu 4,816
Dawa ya uvimbe kwenye kizazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *