Last Updated on 10/03/2023 by Tabibu Fadhili Paulo
Dawa ya P.I.D
P.I.D ni ugonjwa gani?
Maambukizi Katika Mfumo wa Uzazi wa Mwanamke (PID)
Maambukizi katika via vya uzazi vya mwanamke hujulikana kwa kitaalamu kama ‘Pelvic Inflamatory Diseases’ yaani P.I.D
P.I.D ni ugonjwa mpya katika jamii yetu na ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake.
Maambukizi haya huweza kuhusisha shingo ya uzazi, yanaweza kuwa pia kwenye nyama ya mfuko wa uzazi, na katika mirija ya uzazi.
NI NINI HASA HUSABABISHA P.I.D?
Huu ni ugonjwa wa unaotokana na bakteria wanaojulikana kwa kitaalamu bakteria wa jamii ya ‘Neisseria Gonorrhoeae’ na kundi lingine la bakteria hawa hujulikana kama ‘Chlamydia trachomatis’.
Makundi haya mawili ya bakteria ndiyo wanahusika kwa sehemu kubwa na ugonjwa huu wa P.I.D.
JE P.I.D HUAMBUKIZWAJE?
Zipo njia kadhaa ambazo wanawake wanaweza kuambukizwa ugonjwa wa P.I.D.
Baadhi ya hizo njia ni pamoja na:
1. Kushiriki tendo la ndoa bila kinga
2. Maambukizi katika njia ya uzazi baada ya kujifungua
3. Kutoa ujauzito kwa njia zisizo salama
4. Baadhi ya dawa za uzazi wa mpango
5. Kuwa na wapenzi wengi
6. Kuambukizwa kupitia damu yenye vimelea vya PID hasa katika harakati za upasuaji nk.
Dalili za P.I.D
Wapo baadhi ya wanawake ambao wanaweza kuwa na ugonjwa huu na wasionyeshe dalili wala ishara zozote za kuwa nao.
Mwanamke akianza kuonyesha dalili za ugonjwa wa P.I.D anaweza:
1. Kuhisi maumivu ya tumbo hasa maumivu chini ya kitovu
2. Kutokewa na maumivu ya mgongo mara kwa mara
3. Kupata utoko mchafu sehemu za siri ambao huambatana na harufu mbaya kama shombo ya samaki
4. Kupata maumivu wakati wa kukojoa
5. Kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa
6. Kupata damu bila mpangilio akiwa kwenye siku zake
7. Kuwa na homa mara kwa mara
8. Kichefuchefu na
9. Kutapika
Madhara ya P.I.D
P.I.D inaweza kukuletea madhara yafuatayo usipochukuwa hatua ya kutibu tatizo hili mapema
- Inavuruga homoni
- Inavuruga mzunguko wa hedhi
- Inasababisha uke kuwa mkavu
- Inaondoa ute ute wa uzazi (ovulation)
- Mirija ya uzazi itajaa maji
- Mirija ya uzazi kuziba
- Kuvimba mirija ya uzazi
- Inaweza kukuletea saratani ya shingo ya kizazi
- Inaweza kukufanya kuwa mgumba
Je unahitaji dawa ya asili ya kutibu P.I.D? Kama ndiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.
Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili. Ninayo ofisi yangu binafsi Jijini Dar Es Salaam. Lakini nafanya pia kazi kwa njia ya mtandao.
Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni.
Kama unahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kutibu kabisa PID niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.
Natuma pia popote ulipo nje ya Dar, tuwasiliane kwanza WhatsApp.
Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao
To get knowledge