Je unaweza kupata ujauzito wakati unaendelea kutumia dawa za uzazi wa mpango?

Je unaweza kupata ujauzito wakati unaendelea kutumia dawa za uzazi wa mpango?

Last Updated on 11/08/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Je unaweza kupata ujauzito wakati unaendelea kutumia dawa za uzazi wa mpango?

Dawa karibu zote za uzazi wa mpango zile za kizungu na hata za asili zote zina asilimia mpaka 99 tu za kufanya kazi ya kuzuia usipate ujauzito hasa kama zinatumika vizuri na kama inayopaswa.

Ninaposema zinapaswa kutumika vizuri na kama inavyopaswa namaanisha kwamba dawa kama ni ya kutumika kila siku saa fulani basi kweli itumike kila siku na muda ule ule.

Kwa hiyo kama kwa bahati mbaya ikakutokea mara moja moja unasahau kumeza dawa au unameza mida tofauti tofauti basi uwezo wa dawa ya uzazi wa mpango kuzuia usipate ujauzito unaweza kushuka mpaka kufika asilimia 91.

Pamoja na hizo asilimia zote yaani asilimia 99 au 91 za wewe kutoweza kupata ujauzito kwa kutumia dawa za uzazi wa mpango bado kuna uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito wakati unatumia dawa.

Kushindwa huku kwa dawa za uzazi wa mpango kukulinda usipate ujauzito mara nyingi ni matokeo ya kutotumia dawa kwa usahihi kama inavyoagizwa na daktari.

Kama unasahau mara moja au kwa mfululizo siku kadhaa labda unajipa matumaini pengine mmeo amesafiri kidogo kunaweza kufanya homoni zako zikae sawa na tayari kwa ajili ya uzazi.

Ukiacha hilo la kutotumia dawa kwa usahihi pia kuna vitu vingine vinavyoweza kupunguza ufanisi wa dawa za uzazi wa mpango ikiwemo matumizi yaliyozidi ya pombe.

Kunywa pombe kila siku tena kupita kiasi kunaweza kusababisha ini kumeng’enya dawa ya uzazi wa mpango kwa namna ambayo si sahihi na hivyo kuathiri ufanisi wake.

Unashauriwa kutumia njia zingine za uzazi wa mpango za dharura unapokuwa na wasiwasi zaidi wa kupata ujauzito pamoja na kuwa unatumia vidonge vya uzazi wa mpango kama vile kuvaa mpira au kutumia vidonge vinavyotumika kuzuia ujauzito mara moja tu baada ya tendo la ndoa.

Mara zote usitumie dawa yoyote bila uangalizi wa karibu wa Tabibu.

Ikiwa unatafuta dawa nzuri ya asili ya uhakika ya uzazi wa mpango isiyo na madhara kwa sasa wala baadaye niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Ninayo dawa nzuri sana ya asili kwa ajili ya uzazi wa mpango ambayo inatumika mara moja tu kwa mwaka na haina madhara yoyote mabaya.

Bila shaka nimefanikiwa kukujibu swali lako la ikiwa unaweza kupata ujauzito wakati unaendelea kutumia vidonge vya uzazi wa mpango.

Kama utakuwa na swali zaidi unaweza kuuliza hapo chini nitakujibu na wala hulazimiki kutaja jina lako kamili wakati unauliza swali lako.

Kabla hujaondoka soma pia na hii 👇

Je kushiriki tendo la ndoa mara nyingi kunaongeza furaha zaidi?

Imesomwa na watu 225
Je unaweza kupata ujauzito wakati unaendelea kutumia dawa za uzazi wa mpango?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *