Last Updated on 30/08/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Je kutopata mtoto kunakuondolea hamu ya tendo la ndoa?
Nafahamu hilo na sidhani kama hilo ni swali la kuuliza.
Sababu inajulikana wazi kwamba ikiwa umekaa miaka kadhaa na hupati mtoto basi ni jambo la kawaida kabisa kuishiwa hamu ya tendo la ndoa.
Hata hivyo mechi lazima iendelee
Inawezekana mama hatumii tena uzazi wa mpango, inawezekana mmeshavizia sana kutafuta ujauzito katika siku za hatari mara kadhaa bila majibu
Lakini matokeo ni kuwa mpaka sasa mkeo haonyeshi dalili zozote za kuwa na kitambi.
Inawezekana tena na hospitali mmeenda wote wawili na mkafanya na vipimo wote wawili na ikajulikana wazi hakuna tatizo lolote la kiafya linalozuia msipata mtoto lakini bado hakuna ujauzito
Mara kadhaa nimetafutwa na wasomaji wangu wananiambia hawana kabisa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa na kwamba wangehitaji msaada au dawa kwa haraka ili kutatua matatizo hayo
Mwanaume anajikuta uume hautaki tena kusimama, ukisimama upo lege lege na hauna nguvu wala uimara wowote
Mke ameishiwa kabisa hamu na hata akiandaliwa vipi hana msisimko wowote na hafiki tena kileleni hata baba ashinde hapo kifuani masaa mawili
Lakini ninapowahoji hoji baadhi yao wanasema wazi hatuna mtoto na tumeshahangaika na kutafuta mtoto mwaka wa pili au wa tatu sasa bila mafanikio yoyote.
Kwa mwanaume inatokea kama vile uume nao umekuwa na ubongo wake binafsi unaojitegemea ili kuishi.
Hayo nayafahamu na yapo.
Kwa kawaida ili uwe na hamasa ya kutaka kushiriki tendo la ndoa ni lazima akili yako iwe na utulivu wa kutosha na bila mawazo mawazo yoyote.
Kutopata mtoto ni moja ya vitu vinavyoleta msongo wa mawazo kwa baadhi ya wanandoa na matokeo yake wanapoteza kwa pamoja hamu ya kushiriki tendo la ndoa na bila kujua wanadhuru zaidi uwezo wao wa kuweza kupata ujauzito.
Homoni zile zile zinazohusika na mambo ya uzazi ndiyo homoni hizo hizo zinazohusika na kudhibiti msongo wa mawazo mwilini kwako
Mwili unapoona upo na mawazo mawazo sana huzielekeza homoni za uzazi ziende kushughulika kwanza na msongo wa mawazo unaokukabili na siyo kushughulika na uzazi
Ubongo na mwili wako vinaupa kipaumbele zaidi msongo wako wa mawazo kuliko hitaji lako la mtoto.
Kwa hiyo natambua wazi kwamba tatizo lako la kutopata mtoto linakuletea mawazo na mawazo hayo yanakupelekea hata kuishiwa hamu ya tendo la ndoa.
Ushauri wangu kwako leo ni huu > JITAHIDI SANA KADRI UWEZAVYO UIISHI LEO, usiwaze sana KUHUSU JANA AU KUHUSU KESHO.
Ishi leo, furahia muda huu ulionao leo
Kuna mengi sana kwenye maisha ya ndoa zaidi ya watoto.
Mweleze Mungu shida yako, chukua hatua ili kujaribu kupata suluhu ya tatizo lako LAKINI KAMWE USIBADILI TATIZO LAKO KUWA KUBWA KULIKO HATA MUNGU WAKO.
Kwa hiyo kama unakosa hamu ya kushiriki tendo la ndoa sababu hampati mtoto hapo tatizo siyo kutibu hamu ya tendo la ndoa.
Hapo unahitaji kupambana na chanzo cha tatizo ambacho ni mtoto apatikane au uachane na mawazo hayo ya kutaka kupata mtoto kwa sasa na uendelee na maisha mengine.
Endelea kufanya vipimo hospitali nyingine tofauti na uendelee kutumia dawa bila kukata tamaa.
Acheni mawazo, fanyeni mazoezi ya viungo mara kwa mara, pateni muda wa kutosha wa kupumzika na kulala, rahisisha maisha na ratiba zenu.
Maisha ni asilimia 10 ya yale yanayokutokea na asilimia 90 ni vile unavyoyajibu yale yanayokutokea.
Huwezi kuzuia shida zisikutokee bali unao uwezo wa kudhibiti namna unavyozijibu hizo shida.
Kama umekuwa ukitafuta ujauzito kwa kipindi kirefu bila mafanikio na unahitaji dawa nzuri ya asili ya uhakika isiyo na gharama kubwa ya kukusaidia kupata mimba niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175. Maelezo yake zaidi unaweza kuyasoma kwa kubonyeza hapa.
Share na wengine uwapendao.