Last Updated on 15/12/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Namna ya kufahamu mzunguko wako wa hedhi ni wa siku ngapi
Ili kufahamu vizuri ni siku zipi ni hatari kwa mwanamke kupata mimba, unahitaji kwanza kujifunza jinsi mzunguko wa hedhi (menstrual cycle) unavyofanya kazi.
Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa siku ya kwanza wakati mwanamke anaanza kuona siku zake (kublidi) na tunaiita ni siku ya Kwanza.
Baada ya kuuelewa vizuri mzunguko wa hedhi wa mwanamke, tunaweza kuzifahamu siku za kupata mimba mwanamke.
Kimsingi kuna siku 6 ambazo mwanamke anaweza kubeba mimba – siku 5 kabla ya kutoa yai na saa 24 baadaya yai kutolewa.
Hii ni kwa sababu mbegu za mwanamme zina uwezo wa kukaa kwa siku 5 ndani ya mwili wa mwanamke kabla hazijafa na yai (ovum) la mwanamke lina uwezo wa kuishi kwa saa 12 hadi 24.
Mzunguko wa hedhi wa kawaida huwa una sifa madhubuti zifuatazo:
Namna ya kufahamu mzunguko wako wa hedhi ni wa siku ngapi
Soma kwa umakini maelezo haya ili uweze kufahamu mzunguko wako wa hedhi ni wa siku ngapi;
Ikiwa ulianza kuona siku zako tarehe 12/10/2021 (tarehe 12 mwezi wa 10), basi tarehe 12/10/2021 inakuwa siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi.
Na tarehe 13/10/2021 inakuwa siku yako ya pili ya mzunguko wa hedhi
Na teherhe 14/10/2021 inakuwa siku ya tatu kadhalika
Tarehe 15/10//2021 ni siku ya 4
Tarehe 16/10/2021 ni siku ya 5
.
.
Nakuendelea.
Utakoma kuhesabu mzunguko wako wa hedhi mara tu unapopata hedhi nyingine.
Ikiwa utapata hedhi ingine tarehe 10/11/2021, basi siku ya mwisho ya mzunguko wako wa hedhi kwa mwezi wa kumi inakuwa tarehe 09/11/2021, na tarehe 10/11/2021 inakuwa ni siku yako ya kwanza ya mzunguko wa mwezi wa 11
Kufahamu mzunguko huo ni wa siku ngapi hesabu tangu tarehe 12 mwezi wa 10 hadi tarehe 9 mwezi wa 11 ni siku ngapi; jibu ni siku 30 (kwa sababu oktoba 2021 ilikuwa na siku 31, kama ingekuwa ni oktoba ya siku 30 kama miaka mingine mzunguko huo ungekuwa ni wa siku 29).
ZINGATIA mwezi unaweza kuwa na siku 31, 28, 29 au 30, kwa hiyo kama hujui ukubwa mbalimbali wa miezi lazima utumie kalenda yako vizuri.
Kwa hiyo mzunguko wa pili ameanza tarehe 10/11/2021 (tarehe 10 mwezi wa 11) na akaanza kuona siku zake tena kwa mara nyingine tarehe 9/12/201 siku yake ya mwisho ya mzunguko huu ni tarehe 8/12/2021 na mzunguko huu wa pili una siku 29 (unahesabu tangu tarehe 10 novemba hadi tarehe 8 disemba)
Kwanini mizunguko yangu ina idadi ya siku tofauti?
Hili nalo ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la tendo la ndoa kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatari kwa mwanamke kubeba ujauzito.
Kwa mfano nilioweka hapo juu utaona mzunguko wa kwanza alikuwa na mzunguko wa siku 30 wakati mzunguko wa pili alikuwa na mzunguko wa siku 29.
Ili tuhitimishe kwamba mwanamke ana mizunguko ya hedhi iliyo sawa (regular cycles), idadi ya siku za mizunguko ya hedhi haitakiwi itofautiane kwa zaidi ya siku 7.
Na ukiwa na mzunguko wa hedhi wenye tofauti ya zaidi ya siku 7 mana yake mzunguko wako haupo sawa na ni ishara homoni zako zimevurugika.
Mfano, kama mwezi wa kwanza uliona siku zako baada ya siku 28, mwezi wa pili ukaona baada ya siku 30, mwezi wa tatu ukaona baada ya siku 35 na mwezi wa nne ukaona baada ya siku 21, bado mzunguko wako uko kwenye uwiano mzuri (regular cycle) kwa kuwa mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.
Hivyo usikariri kwamba siku za mzunguko wa hedhi kwa kila mwanamke ni siku 28, hilo halipo. Hizi siku 28 ni wastani tu.
Wengine wanaona siku zao kila baada ya siku 21, wengine kila baada ya siku 25, wengine 29, wengine 35 na bado tunasema mizunguko yao bado ni mizunguko ya kawaida.
Pia fahamu ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyo huyo. Mfano usitarajie kuwa kama mwezi wa tatu (march) ameona siku zake baada ya siku 28 na mwezi wa nne (april) pia ataona siku zake baada ya siku 28. Si lazima itokee hivyo lakini pia huwa inaweza kutokea.
Mfano, mwanamke mmoja mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28, mzunguko unaofuata baada ya siku 27, mzunguko mwingine baada ya siku 30, mzunguko mwingine baada ya siku 29, mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa kwa kuwa tofauti si zaidi ya siku 7 kama nilivyoeleza hapo juu.
Idadi ya siku za kuona siku zake na idadi ya ya siku za mzunguko wa hedhi
Usichanganye kati ya siku za hedhi (menstrual period) na mzunguko wa hedhi (menstrual cycle) kwani hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.
Siku ya kwanza ya kuona siku zako ndiyo siku tunaanza kuhesabu mzunguko wako wa hedhi (day one) na siyo siku ya kumaliza kuona siku zako (kublidi) kama wengi wanavyodhani.
Kawaida idadi ya siku za siku zako unazoona damu ni kati ya siku 3 mpaka 7.
Kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo.
Mwingine anaenda siku 3 amemaliza, mwingine siku 4, mwingine 5 mwingine 6 mpaka 7.
Chochote zaidi ya siku 7 si cha kawaida na unahitaji kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi.
Picha ifuatayo inaonyesha kila mzunguko na siku yake ya kupata ujauzito
Ikiwa utahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175 maelezo yake zaidi unaweza kusoma hapa.
Nlikuwa nauliza hivi sasa Kama mizunguko ya hedhi inatofautiana sasa utajuaje siku zako za hatari na wakati Mara 30,29,28,21
Weka Sawa kwanza mzunguko wako. Hiyo yaweza kuwa ni dalili homoni zako zimevurugika