Last Updated on 22/08/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Rais wa Urusi alitoa agizo wiki hii akiboresha tuzo inyoitwa “Mothers of Veterans”, ambayo ilianzishwa mwaka 1944 na serikali ya Umoja wa Kisovieti.
Tuzo hii inalenga kuhamasisha familia kuwa na watoto wengi zaidi.
Rais Putin alisema wiki hii kwamba tuzo hiyo ambayo inaendana na fedha na vitu vingine vya thamani itatolewa kwa kila mama atakayejifungua watoto 10 na kuendelea.
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kukabiliana na kupungua kwa kasi ya ongezeko la watu nchini Urusi.
Vyombo vya habari vya kimataifa, vikiwemo magazeti ya Washington Post na Express, vilitangaza habari hii kuhusu agizo hilo la rais wa Urusi, ambalo limeleta mjadala mkubwa kimataifa.
Rais huyo amechukua hatua hii wakati jeshi la Urusi likiwa vitani nchini Ukraine baada ya kuanzisha mashambulizi mwishoni mwa Februari mwaka huu.
Inadaiwa wanajeshi 15,000 wa Urusi wameuawa hadi sasa katika vita vya Ukraine na wengine takriban 45,000 wamejeruhiwa.
Hata hivyo, tuzo hii haihusiani na athari za vita nchini Ukraine.
Mbali na Urusi, kuna nchi nyingine 4 duniani ambazo zinazohimiza familia kuwa na watoto wengi, ambazo baadhi yao huwaahidi wazazi pesa na malezi ya watoto, kama ilivyoonyeshwa katika makala iliyochapishwa na gazeti la Money.
2. Finland
Finland, moja ya nchi za Ulaya zenye idadi ndogo zaidi ya watoto wachanga, inalipa pesa za ziada kwa watu ili kupata watoto.
Tangu mwaka 2013, kila mtoto aliyezaliwa katika wa mji Lestijärvi amepewa €10,000 kupitia kwa mama yake.
Lestijärvi ni mojawapo ya miji yenye watu wachache zaidi nchini Finland.
3. Estonia
Estonia, moja ya nchi za Ulaya ambayo kwa muda sasa imekuwa ikitumia pesa kuongeza idadi ya watoto wanaozaliwa, na serikali inafurahia hasa familia zenye watoto wengi zaidi.
Familia ya Kiestonia yenye watoto watatu hulipwa €520 kwa mwezi, jambo ambalo huwatia moyo watu ‘kupambana’ kupata watoto wengi zaidi.
Nchi hii imeweza kuongeza idadi ya watoto waliozaliwa katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.
4. Japan
Nchini Japani, idadi ya watoto wachanga wanaozaliwa imefikia kiwango cha chini kabisa katika miaka ishirini na minne iliyopita, kulingana na Business Insider.
Lakini maeneo ambayo yamepiga hatua kubwa katika idadi ya wanaojifungua ni maeneo ambayo pesa za bonasi hulipwa kwa akina mama wanaojifungua watoto wapya.
Katika mojawapo ya majiji nchini humo, yanayoitwa Ama, ambayo ni sehemu ya kisiwa cha Nakanoshima, kila mzazi anayejifungua mtoto wake wa kwanza hupewa kiasi cha yen 100,000 (sawa na dola 940).
Wanapofikia mtoto wa nne wanalipwa yen milioni 1 (sawa na dola zipatazo 9,400).
5. Australia
Gazeti la Money lilisema kwamba Australia ni mojawapo ya nchi zinazojitahidi kuongeza idadi ya watoto wanaozaliwa, ingawa hakuna kiasi maalum kinachotolewa kwa wazazi wa mtoto mchanga.
Lakini nchi hii ni miongoni mwa nchi zinazotoa huduma binafsi kwa wazazi ambao wana watoto, ambapo serikali inasaidia kwa mambo mengi kwenye eneo la huduma kwa watoto.
Mpendwa hapo mchawi ni passport (hati ya kusafiria nje ya nchi) na Visa.
Kama unahitaji dawa ya asili inayoweza kukusaidia kupata ujauzito bonyeza tu hapa.