Last Updated on 07/12/2023 by Tabibu Fadhili Paulo
Chakula sahihi kwa mama anayenyonyesha
Mama anayenyonyesha ni lazima apate chakula sahihi kwake na cha kutosha.
Hii ni kwa sababu chakula anachokula hakimhusu yeye peke yake bali kinamhusu pia mtoto anayenyonyesha.
Katika muda wote wa masaa 24 mwili wa mama anayenyonyesha huwa upo bize ukitengeneza maziwa ambayo ndicho chakula cha mtoto.
Katika kufanya kazi hiyo mwili unahitaji upewe chakula sahihi na cha kutosha.
Siyo chakula sahihi tu bali kiwe pia ni cha kutosha.
Ni jambo la kawaida sana kumkuta mama anayenyonyesha akiwa na njaa wakati wote, hii inatokana na shughuli hiyo nzito ya kuzalisha maziwa kwa ajili ya mtoto.
Hivyo mama mjamzito apewe chakula sahihi, chakula cha kutosha na akingwe asiwe na mawazo mawazo yoyote (yaani asiwe na stress yoyote).
Vyakula ninavyoviandika hapa vinatajwa ni msaada mkubwa kwenye kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa mama na utaona vingi kati ya hivyo vina protini nyingi hasa protini ya asili.
Ili kuongeza uwezekano wa kuzalisha maziwa ya kutosha na kuwa na afya bora wakati wote wa kunyonyesha mama mjamzito ahakikishe kwenye chakula chake cha kila siku kimojawapo au viwili mpaka vitatu ya vyakula vifuatavyo havikosekani ;
1. Mbegu za maboga au Unga wake
2. Korosho
3. Karanga
4. Ufuta
5. Parachichi
6. Unga wa majani ya mlonge
7. Uyoga
8. Samaki
9. Mboga za majani
10. Chia seeds
11. Kweme
12. Uji wa Unga wa ndizi
13. Nazi
14. Maharage na vyakula vyote jamii ya kunde
15. Maji ya kunywa
Kuna mtu anauliza vipi kuhusu wali?
Wali au ugali hata pizza unaruhusiwa kula ila asilimia 75 ya mlo wako uhusishe hivyo nilivyoviorodhesha hapo juu.
Kwa wale wanaonunua dawa ya asili kwangu kwa ajili ya kupata ujauzito huwa nawaeleza kila kitu kuhusu chakula chao wakati wa kutafuta ujauzito, wakati wa ujauzito na wakati wa kunyonyesha.
Kama na wewe unapenda miongozo hiyo kuhusu vyakula, nunua tu dawa kutoka kwangu na utakuwa rafiki yangu na mtu wangu wa nguvu.
Tuwasiliane WhatsApp +255714800175