Je PID ni ugonjwa wa zinaa?

Last Updated on 13/05/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Je PID ni ugonjwa wa zinaa?

Huenda ukawa unajiuliza bila kupata majibu sahihi ikiwa PID ni ugonjwa wa zinaa au la…

Kwenye makala hii nitakufafanulia juu ya hili na utakuwa na amani hatimaye.

PID ni kifupi cha maneno ya kiingereza yanayosomeka kama ‘Pelvic Inflammatory Disease‘.

Kwa Kiswahili rahisi PID ni maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke.

Tunaposema ugonjwa fulani ni ugonjwa wa zinaa tunamaanisha ugonjwa huo umetokana na kujamiana kati ya mwanaume na mwanamke na mmoja kati yao amemwambukiza mwenzake.

Kwa kiingereza magonjwa ya zinaa hujulikana kama STDs yaani ‘sexual transmitted diseases’.

Kumbe PID yenyewe siyo ugonjwa unaoweza kuupata moja kwa moja kama matokeo ya kushiriki tendo la ndoa.

Je PID ni ugonjwa wa zinaa?

PID ni maambukizi kwenye mji wa uzazi wa mwanamke, vimelea vya magonjwa mengine ya zinaa kama vile klamyadia, kaswende na Kisonono au hata vya u.t.i sugu vinapouingia mji wa uzazi wa mwanamke ndipo kunatokea ugonjwa wa P.I.D.

Kwahiyo mpaka hapo utaona kwamba hatuwezi kuuweka ugonjwa wa P.I.D moja kwa moja kwenye kundi la magonjwa ya zinaa bali ni matokeo ya pili ya magonjwa ya zinaa mwilini kwa mwanamke.

Moja ya madhara ya wazi ya PID ni mwanamke kushindwa kushika ujauzito kirahisi na kupoteza hamu yake ya asili ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

Mwanamke pia hutokwa na uchafu ukeni wenye rangi ya kahawia na wenye harufu ya kukera inayomuondolea hali ya kujiamini.

Kama ulikuwa unawaza kama ugonjwa wako wa PID ni ugonjwa wa zinaa au la, basi nimekupa jibu kwamba siyo ugonjwa wa zinaa bali ni ugonjwa unaotokana na matokeo na magonjwa ya zinaa na unaathiri hasa viungo vya uzazi vya ndani ya mwanamke.

Je PID ni ugonjwa wa zinaa?

Ili kutibu PID ni vizuri wenza wote wawili mme na mke wapatiwe matibabu hasa yanayodhibiti bakteria na virusi na maambukizi mbalimbali mwilini na ikiwezekana mama asishiriki tendo la ndoa mpaka amepona kabisa tatizo lake.

Ikiwa umekuwa ukihangaika kwa muda mrefu na ugonjwa huu wa PID na unahitaji kutumia dawa ya asili kwa ajili hiyo niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili kutoka Tumaini Herbal Life iliyopo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

Imesomwa na watu 20
Je PID ni ugonjwa wa zinaa?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *