Last Updated on 21/06/2024 by Tabibu Fadhili Paulo
Jinsi ya kupata ujauzito kwa haraka
Kwenye makala hii naeleza kwa kirefu jinsi ya kupata ujauzito kwa haraka.
Nitazijadili baadhi ya njia rahisi za kupata ujauzito kwa haraka.
Fuatana na mimi mpaka mwisho.
Naitwa Fadhili Paulo ni Tabibu wa Tiba asili, napatikana Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.
Ikiwa umekuwa ukitafuta mbinu za kukusaidia kupata ujauzito kwa haraka au kirahisi, basi makala hii itajibu shauku ya hitaji lako.
Ukweli ni kuwa njia rahisi kabisa ya kupata ujauzito haraka ni kuwa na mme nyumbani kwako!
Ndiyo, nimesema njia rahisi ya kupata ujauzito ni kuwa na mme nyumbani kwako unapoishi.
Kama unaishi nyumba moja na mmeo wala hupati shida kuanza kujiuliza ni jinsi gani utapata ujauzito, utaona tu automatic umepata ujauzito.
Huhitaji kujua chochote.
Ukiona umeanza kutaka kusoma na kufahamu ni jinsi gani utapata mimba, basi ujue kuna kitu hakipo sawa mahali fulani kwenye mfumo wako wa uzazi au hauishi nyumba moja na mme unayetaka kuzaa naye.
Hata hivyo usinielewe vibaya na sina lengo lolote baya juu yako.
Hapa chini nimekuandalia njia 7 unazoweza kuzifuata na ukafanikiwa na hitaji lako la kutaka kupata ujauzito haraka ;
Jinsi ya kupata ujauzito kwa haraka
1. Acha kutumia dawa za uzazi wa mpango
Kama unahitaji kupata ujauzito haraka ni mhimu sana uache matumizi ya dawa za uzazi wa mpango miezi kadhaa kabla.
Hapa inashauriwa usitumie dawa au kitu kingine chochote kinachoweza kutumia kama uzazi wa mpango (dawa, sindano, vipandikizi nk).
Itafaa uchukue uamuzi huu miezi mitatu au hata miezi sita kabla.
Kama umekuwa ukitumia dawa za uzazi wa mpango kwa muda mrefu basi tambua inaweza kuchukua muda zaidi kupotea ndani ya mwili wako hata baada ya kuacha kuzitumia na hivyo mifumo yako ya homoni mwilini itahitaji muda zaidi ili kurudi na kukaa sawa kama zamani.
Hata hivyo wapo baadhi ya wanawake ambao wanabahatika kupata ujauzito mara baada tu ya kuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango.
Kwahiyo usihitimishe kwamba kwa sababu umekuwa ukitumia dawa za uzazi wa mpango basi zitakusababishia kuchelewa kupata ujauzito.
Ili kuongeza tu uwezekano wa kupata ujauzito kwa haraka au kwa njia rahisi basi unashauriwa kuacha matumizi ya dawa hizo mapema.
2. Pata kujua siku zako za hatari
Kwa bahati mbaya wanawake wengi hawafahamu siku zao hasa za kushika ujauzito ni zipi na zipi hasa.
Hili linachangiwa kwa sehemu kubwa kama matokeo ya homoni kutokuwa sawa hali inayopelekea mwanamke kuona siku zake tarehe tofauti tofauti na wakati mwingine kutokuona kabisa hata kwa miezi kadhaa mfululizo.
Katika hali kama hii ni vigumu kufahamu siku zako zenye uwezekano mkubwa wa kushika ujauzito.
Hata hivyo kama unatafuta mbinu za kukusaidia kupata mimba haraka bado unatakiwa uwe na uelewa mkubwa kuhusu siku zako na mzunguko wako wa hedhi kwa ujumla.
Kwa sababu hii mara nyingi nashauri upende kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara hata zile siku ambazo siyo siku za hatari kwa mjibu wa uelewa wako.
Inapendekezwa mtu aliyebize kutafuta ujauzito ashiriki tendo la ndoa kila baada ya siku 1 ili kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito.
Kwahiyo ni mhimu uishi nyumba moja na mmeo wakati unatafuta ujauzito.
Tabia ya mwanamke kuwa Mbeya mwanaume kuwa Arusha halafu mnaonana mara moja kwa mwezi itawasababishia kuchelewa sana kupata mtoto.
Wakati huo huo nasisitiza mara nyingi watu kutokuwa na wazo kichwani la lazima wapate ujauzito wakati wanashiriki tendo la ndoa.
Wewe shiriki tendo la ndoa mara nyingi hata siku zisizo za hatari lakini fanya hivyo kama sehemu ya burudani na siyo umeshikilia kichwani kwamba lazima upate ujauzito.
Kama mzunguko wako haueleweki vizuri na siku zako za hatari hazijulikani basi usione tabu kutoa hela kidogo kwa daktari akusaidie kubaini siku zako hasa ni zipi, tatizo baadhi yenu mnapenda kila kitu mpate BURE.
3. Shiriki tendo la ndoa siku chache kabla ya kuona ute wa uzazi
Kama unataka kupata ujauzito haraka basi kushiriki tendo la ndoa siku chache kabla hujaanza kuuona ute wa uzazi kunaongeza uwezekano wa wewe kupata ujauzito.
Hii inatokana na ukweli kwamba mbegu za mwanaume zinaweza kuendelea kuwa hai ukeni kwako siku 3 au hata 5 baada ya kushiriki tendo la ndoa.
Hivyo unaposhiriki tendo la ndoa siku chache kabla ya kuona ute wako wa uzazi kunafanya mbegu iwepo hapo na kukutana na yai wakati wowote litakaposhuka tayari kwa kurutubishwa kwa kuwa yai la mwanamke linaweza kubaki hai na kufaa kwa kurutubishwa masaa 12 mpaka 24 tu tangu lishuke.
Kwahiyo unaposhiriki siku chache kabla ya kuanza kuona ute wako wa uzazi ni kama kujiweka tayari wakati wowote yai na mbegu vikutane hata kama wakati huo haushiriki tendo.
Kama ute wako wa uzazi wenyewe huuoni au hujuwi upoje basi inashauriwa ushiriki tendo la ndoa mara kadhaa katika wiki mara tu baada ya siku zako za hedhi kuisha hasa kama mzunguko wako haueleweki na unabadilika kila mara.
4. Baki kitandani baada ya tendo la ndoa
Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kuthibitisha hili, bado nakushauri ubaki kitandani ukiwa umelalia mgongo mara baada ya kumaliza tendo la ndoa na mwenza wako.
Kuendelea kubaki kitandani umelalia mgongo kunakuhakikishia mbegu nyingi za mwanaume kuendelea kutafuta na kufuata yai lako kwa muda mrefu na kukuhakikishia kupata ujauzito.
Baada ya tendo la ndoa baki kitandani dakika 15 hata 20 ndipo uinuke.
Na kwa sababu hii napendekeza ushiriki tendo la ndoa usiku kabla ya kwenda kulala kwani kunakuhakikishia unabaki kitandani muda mrefu tofauti na asubuhi labda utataka uwahi kuamka uandae chakula au uelekee kazini.
Mhimu hapa mmeo asiwe na uchovu mwingi hata wewe mwenyewe usiwe una dalili za kuchoka choka sana kabla hamjaingia kulala.
Wakati hakuna ushahidi wa kisayansi kuhusu hili bado staili ya zamani na ya miaka yote ya mwanamke kulala chini na mwanaume juu bado ndiyo staili ya uhakika zaidi ya kukusaidia kupata ujauzito kirahisi.
5. Acha vifuatavyo
Wakati upo bize kutaka kupata mimba haraka ni mhimu kufahamu kwamba kuna aina fulani ya maisha utatakiwa kuyaacha kwa muda.
Kama upo bize sana kutaka kupata ujauzito haraka utatakiwa kuacha kunywa chai ya rangi, kahawa, soda yoyote, juisi yoyote ya dukani, kuvuta sigara, kuacha pombe na kilevi kingine chochote.
Utatakiwa kuacha pia kushiriki mazoezi mazito ya viungo.
Fanya mazoezi madogo madogo ya kawaida kama vile yale ya kutembea tembea na kusimama hapa na pale.
Mazoezi mazito kama vile kukimbia mbio kwa muda mrefu yanaweza kukuchelewesha kushika mimba.
Jitahidi uache kula vyakula feki au vya kisasa zaidi maarufu kama ‘fast foods’.
Kula vyakula vya asili zaidi huku ukitumia mboga nyingi za majani.
Mboga za majani zisiive sana, kama unaweza kupata mboga ya majani unayoweza kula ikiwa mbichi bila kupikwa itumie hiyo zaidi.
6. Fanya kipimo cha ujauzito mara kwa mara
Ikiwa unahitaji kupata ujauzito haraka unaweza kuwa unajiuliza ni muda gani uchukue kipimo kuona kama umepata ujauzito au la.
Jibu ni kuwa wiki 1 au 2 za kutoka ulipokosa kuona siku zako unaweza kupima.
Vipo vipimo vidogo vinapatikana kwenye maduka ya madawa unaweza kununua hivyo na kujipima mwenyewe.
Unapofanikiwa kujigundua mapema kuwa ni mjamzito Itakusaidia kukupa hamasa ya kumtafuta daktari kwa msaada zaidi juu ya namna ya kuishi mara baada ya kupata ujauzito ili kupunguza uwezekano wa ujauzito huo kukutoka kizembe Kutokana na kuishi tofauti na inavyotakiwa mama mjamzito kuishi.
7. Tafuta ujauzito tena na tena
Haijalishi unahitaji kupata ujauzito kwa haraka kiasi gani, bado hakuna muujiza wa haraka kwenye maisha yetu ya hapa duniani.
Ni muda gani itakuchukua kupata ujauzito ni swali lenye majibu tofauti kwa kila mwanamke.
Utatakiwa kuwa mvumilivu na zaidi ya yote hutakiwi kuwaza sana kwanini hupati ujauzito kwa wakati huo unaotaka.
Kuna mambo mengine mengi yanayohitajika hapa ili upate ujauzito ikiwemo umri wako wa Sasa na hali ya afya yako wewe mwanamke na ya mmeo.
Ingawa upo uwezekano wa wewe kupata ujauzito kwenye jaribio lako la kwanza la kutaka kupata ujauzito, bado hakuna uhakika kwamba utapata.
Utatakiwa kujaribu tena na tena mpaka upate unachokitafuta.
Lakini kama inapita mwaka mmoja na hakuna matokeo unayoyahitaji basi ni vizuri ukifanya vipimo kuona kuna kitu gani hasa kinachozuia usipate ujauzito na ni vizuri mkipima wote wawili wewe na mmeo.
Nashukuru kwa muda wako.
Na ikiwa umeshafanya hayo yote na bado majibu hayaonekani basi napenda kukujulisha kuwa ninayo dawa nzuri sana ya asili kwa ajili ya kukusaidia kupata ujauzito haraka inaitwa uzazi mjarabu na nimekuwekea maelezo yake hapa chini kama ifuatavyo :
DAWA YA ASILI YA KUPATA MIMBA HARAKA
Hii ni dawa ya asili ya kupata mimba haraka inayosaidia pia kuweka sawa homoni, kuondoa uvimbe kwenye kizazi, kupevusha mayai, kuzuia ujauzito usitoke, kutibu chango la uzazi, kuzibua mirija ya uzazi, kutibu maambukizi kwenye kizazi (PID) na matatizo mengine mengi ya uzazi kwa pamoja.
Uzazi Mjarabu ni dawa ya asili yenye mchanganyiko wa mitishamba na mimea mbalimbali ya asili maalumu kwa ajili ya kutibu matatizo mbalimbali ya uzazi na kukuwezesha kupata ujauzito.
Ni dawa ya asili yenye uwezo wa kutibu matatizo mbalimbali yanayosababisha ugumba kwa pamoja.
Inasaidia kuweka sawa homoni, kuondoa uvimbe kwenye kizazi, kupevusha mayai, kuzuia ujauzito usiharibike, kuzibua mirija, kutibu maambukizi kwenye kizazi, kutoa sumu mwilini, kuleta ute wa uzazi na mengine mengi kwa pamoja.
Dawa hii ina viinilishe, madini na vitamini zote mhimu kwa ajili ya kutungisha mimba kama ifuatavyo;
Uzazi mjarabu ina:
1. Vitamini B6
Kazi kubwa ya vitamini B6 ni kusaidia mimba kukaa sawa na salama wiki mbili za mwanzo tangu ujauzito utungwe (Luteal phase).
Hiki ni kipindi cha maandalizi cha kipindi kingine kijacho katika safari ya ujauzito na ni lazima mazingira yawe ya afya katika mji wa uzazi wa mwanamke ili kweli ujauzito uendelee kukua.
Hivyo siku hizi 14 za mwanzo vitamini B6 ni ya mhimu ili ujauzito ubaki na afya.
Kama huna hii vitamini vya kutosha basi hizi siku 14 hazitafika na ndani ya siku 7 au 10 ujauzito utakutoka.
2. Vitamini B12
Vitamini B12 ni vitamini mhimu sababu husaidia kuweka sawa homoni. Kama matokeo yake inakusaidia kupata siku zako vizuri na kama siku zako zinaenda vizuri basi ni rahisi pia kwako kupata ujauzito wenye utulivu na afya bora ya mtoto.
Vitamini hii ni mhimu pia kwa baba kwani husaidia kumpa mwanaume mbegu nyingi na zenye ubora wa kutungisha mimba.
3. Vitamini C
Vitamini C imekuwa ikihusishwa na uzazi kwakuwa inasaidia kuweka sawa homoni na kukupa mzunguko mzuri wa hedhi vitu ambavyo ni mhimu ili uwe na afya ya kuweza kupata ujauzito.
Hii ni vitamini mhimu kwa kinamama ambao wamekuwa wakitumia dawa za uzazi wa mpango kwa kipindi kirefu. Husaidia mji wa uzazi uwe tayari na sawa kwa ajili ya kutunga ujauzito.
Vitamini hii inaisapoti homoni ya ujazi ijulikanayo kama ‘progesterone’ katika mwili na kuimarisha kuta za mji wa uzazi baada ya mimba kutungwa.
4. Vitamini D
Upungufu wa Vitamini D umekuwa ukihusishwa na ugumba moja kwa moja.
Tafiti zinaonyesha upungufu wa vitamini D unaathiri tishu au ogani za uzazi za mwanamke kwamba ogani hizo haziwezi kufanya kazi kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya.
Vitamini D pia ina umhimu mkubwa katika kukua kwa seli na ufanyaji kazi wake. Tafiti zinaonyesha wanawake wenye vitamini D ya kutosha wanakuwa na mji wa uzazi mzuri na wenye afya.
5. Vitamini E
Bila Vitamini E ni vigumu kupata ujauzito. Hii ni vitamini mhimu katika kulinda afya ya seli zetu na hufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini na hivyo kuzilinda seli zisidhurike kirahisi.
Hii inajumuisha seli za mayai ya uzazi, kuta zinazozunguka yai zimetengenezwa kwa vitamini E.
Vitamini E pia husaidia kuweka sawa mbegu za mwanaume kwa kuongeza wingi na ubora wake kwa ajili ya uzazi.
6. Madini ya Folate
Kuwa na kiasi cha kutosha cha madini haya ni jambo la mhimu ikiwa unahangaika kupata ujauzito. Madini haya ni mhimu ili kuzuia ujauzito usitoke.
Ni mhimu mwili uwe na madini haya mapema wakati wowote unapojiandaa kushika ujauzito.
Ukisubiri mpaka upate ujauzito ndiyo uanze kutafuta haya madini tayari utakuwa umeshachelewa.
7. Madini ya chuma
Madini ya chuma yana uhusiano wa moja kwa moja na uzazi. Yanahitajika ili kuzizalisha homoni mbili mhimu za uzazi ambazo ni estrogen na progesterone, ambazo ni homoni mhimu kwa utungaji wa kawaida wa ujauzito.
Tafiti zinaonyesha wanawake wenye kiasi kidogo cha madini haya mwilini mwao wanapata wakati mgumu katika kushika ujauzito.
Mara tu upatapo ujauzito madini ya chuma ni ya mhimu sana ili kuwa na ujauzito wenye afya kipindi chote cha miezi 9.
8. Omega-3 na Omega-6
Haya hujulikana kama mafuta mazuri (good fats). Kumbuka siyo kila mafuta ni mabaya kwa mwili wako, yapo mafuta mazuri na ambayo yanahitajika na mwili wako ili kuwa na afya bora.
Omega-3 na Omega-6 husaidia kuweka sawa homoni zako na kuzifanya zifanye kazi kwa usahihi jambo linalohamasisha uhakika wa kuwa na uwezo wa kutunga kwa mimba na kuwezesha damu kusambaa vizuri kwenye ogani za uzazi.
9. Madini ya Selenium
Selenium ni madini madogo ambayo hufanya kazi kama kiondoa sumu mwilini na hivyo kuimarisha ubora wa seli zetu.
Pia ni madini mhimu kwa ajili ya uundwaji wa mayai na hudhibiti kazi za tezi ya thyroid, tezi ambayo ni mhimu kwa uzalishwaji na uwekaji sawa wa homoni.
10. Madini ya Zinki
Madini ya zinki ni mhimu kwa pande zote mbili kwa mwanamke na mwanaume. Kwa wanawake zinki husaidia uzalishwaji wa mayai na kuyaweka mayai yenye afya na kuweka sawa homoni.
Upungufu wa madini ya zinki pia unahusishwa na mimba kuharibika katika wiki za mwanzo mwanzo tangu kutungwa kwake.
Hivyo kama umekuwa na bahati ya kupata ujauzito halafu haichukuwi muda zinatoka kuna uwezekano mkubwa una kiasi kidogo cha madini ya zinki kwenye mwili wako.
Dawa hii inaweza kutumika na mwanamke yeyote ambaye amekuwa akitafuta ujauzito bila mafanikio iwe anajua sababu za tatizo au hata kama hospitali wanasema kila kitu kipo sawa lakini hupati ujauzito
Kwa kifupi Uzazi mjarabu :
Inatibu matatizo mengi ya Uzazi kwa pamoja na kusaidia kupata ujauzito
*Inaweka sawa homoni
*Inaweka sawa mzunguko wa hedhi
*Inaondoa uvimbe
*Inaimarisha afya ya mayai
*Inatibu chango la Uzazi
*Inazuia mimba kutoka
*Inazibua mirija ya mayai
*Inatibu maambukizi kwenye mji wa uzazi (PID)
*Inaleta ute wa uzazi
*Inasogeza kizazi
*Inaondoa sumu au takataka zozote zisizohitajika kwenye mfumo wa uzazi na mwilini kwa ujumla
Kama unahitaji Uzazi Mjarabu kwa ajili ya kutibu matatizo mbalimbali ya uzazi na kupata ujauzito niachie ujumbe WhatsApp +255714800175.
Uzazi mjarabu inagharimu 140,000 (laki 1 na elfu 40 ) ni ya kunywa kwa miezi miwili.
Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni.
Kwa Dar Es Salaam tunaweza pia kukuletea mpaka ulipo kama utataka, unalipa nauli ya daladala.
Natuma pia popote ulipo nje ya Dar Es Salaam ndani ya Tanzania, tuwasiliane kwenye WhatsApp +255714800175.
Ni mhimu pia ufahamu kwamba baadhi ya matatizo ya uzazi hayatibiki hata upate dawa kutoka wapi, mfano kama una makovu kwenye kizazi au umeshatoa mimba nyingi kabla na mengine mengi wewe mwenyewe unajua.
Dawa inatibu matatizo yanayoweza kukuzuia usipate ujauzito lakini suala la kupata ujauzito tunamwachia Mungu.
Ninao watu wengi waliotumia Uzazi mjarabu na wamepata mafanikio mazuri.
Share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.