Style za kupata mimba

Last Updated on 19/11/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

Style za kupata mimba

Kwenye makala hii naeleza kwa kina ni staili gani hasa ya tendo la ndoa inaweza kukusaidia kupata mimba.

Kama umekuwa ukijiuliza ni staili gani hasa ya tendo la ndoa inaweza kukusaidia kupata ujauzito kwa haraka, basi leo ndiyo mwisho wa tatizo lako.

Unapotaka kupata ujauzito kwa kawaida wewe na mwenza wako mtataka kufanya kila mbinu za kuwasaidia kupata huo ujauzito haraka.

Moja ya mbinu hizo mnazoweza kuwa mnazipeleleza ni iwapo kuna staili fulani ya kushiriki tendo la ndoa inayoweza kusaidia kuleta ujauzito kwa haraka.

Je kufanya tendo la ndoa kwa style fulani kunaweza kusaidia kupata mimba?

Ukweli ni kuwa hakuna staili ya aina yoyote ambayo imethibitika kisayansi kwamba inaweza kukusaidia au kukuwezesha kupata ujauzito!

Ukiona tayari umeanza kutafuta au kupeleleza ni staili gani hasa ya tendo la ndoa inaweza kukusaidia kupata ujauzito ujue tayari kuna kitu siyo sawa kwenye mfumo wako wa uzazi na ni vema kufanya vipimo kubaini ni nini hasa kinazuia usipate ujauzito.

Kama wewe ni wa kupata ujauzito basi huhitaji kujua ni staili gani hasa ya tendo la ndoa inaweza kukusaidia kupata ujauzito, wala huhitaji kujua ni siku gani hasa ndiyo siku ya hatari kwa wewe kupata ujauzito.

Kama huna tatizo lolote kwenye mfumo wako wa uzazi na unaishi nyumba moja na mwenza wako, utaona tu umepata ujauzito bila kuhitaji kujua style wala siku ya hatari.

Kwa Kawaida unaweza kupata ujauzito kwa staili yoyote ya kushiriki tendo la ndoa, hata kama mtashiriki mkiwa mmesimama bado kama wewe ni wa kupata mimba utapata tu!

Mwanaume akitoa goli moja linaweza kuwa na mbegu milioni 15 mpaka milioni 200 na inahitajika mbegu 1 tu kati ya hizo zote ili kutungisha ujauzito.

Kwahiyo ukichunguza vizuri utaona kuwa aina ya style mnayotumia wakati mnashiriki tendo la ndoa haina uhusiano wowote na wewe kupata au kutopata ujauzito!

Hata hivyo kuna staili kadhaa mnaweza kujaribu zinazoonekana zinaweza kukusaidia kupata ujauzito kwa haraka na nitazieleza hapo chini kwa kirefu.

Kinachotokea ni kuwa hizi style zinaruhusu mwingiliano wa karibu kati ya uume na mahali ulipo mji wa uzazi.

Na hivyo kwa kushiriki tendo la ndoa ukitumia mojawapo ya hizi style, mbegu za mwanaume zinaweza kufika sehemu zinapohitajika kwa haraka na kufanya utungishaji wa mimba.

Style za kupata mimba

1. Staili ya kifo cha mende

Style ya kifo cha mende

 

Hii ni ile style ya kushiriki tendo la ndoa ambayo kila mtu anaifahamu.

Ni ile ya asili kabisa yaani ya mwanamke kuwa chini na mwanaume kuwa juu.

Ni ile maarufu kabisa kila mtu anaifahamu, kwa kiingereza hujulikana kama “missionary style”.

Hii ni aina ya staili ya tendo la ndoa ambayo inarahisisha mwingiliano mkubwa (deep penetration).

Inashauriwa mwanamke asiamke haraka baada ya tendo la ndoa ili kuendelea kuruhusu mbegu kwenda kwenye mji wa uzazi kirahisi zaidi.

Mwamamke abaki kitandani bila kuinuka walau kwa dakika 15.

2. Staili ya mbwa

Style ya mbwa

Hii ni staili nyingine inayoweza kukusaidia kushiriki tendo la ndoa huku uume ukiwa karibu sana na mahali pa kuelekea kwenye mji wa uzazi wa mwanamke (cervix).

Ni style maarufu sana ikijulikana kwa kiingereza kama “dog style”.

Hapa mwanamke atapiga magoti na kuinamisha kichwa chini na kufungasha mikono, mwanaume atakuja nyuma yake na kumwingilia mwanamke kama vile mbwa wanavyofanya tendo la ndoa, mwanaume pia atakuwa amepiga magoti kama mwanamke.

Kwa style hii uume utaonekana mkubwa kwa mwanamke na utamfikia ndani kabisa karibu na njia kuelekea kwenye mji wa Uzazi.

Style hii inaweza kufanyika pia wenza wote wawili wakiwa wamesimama huku mwanamke akiinama kidogo akishika ukuta au kiti.

3. Style ya miguu mabegani

Style ya miguu mabegani

Hii ni staili nyingine ya kukusaidia kufanya tendo la ndoa kwa mwingiliano mkubwa (deep penetration).

Kwenye staili hii mwanamke analala kawaida kama vile kwenye staili ya kifo cha mende lakini anainua miguu juu na kuipachika juu ya mabega ya mwanaume.

Miguu mabegani hujulikana pia kwa kiingereza kama ‘The seashell style’.

Ni staili inayomchosha kwa haraka sana mwanamke hivyo inashauriwa kutumia kwa dakika kadhaa tu ili kupunguza maumivu kwa aliyechini.

Hizo ni staili 3 nimependa kuzielezea na ninaamini zinakutosha, ikiwa utahitaji nyingine zaidi niachie ujumbe kwenye WhatsApp +255714800175 nitakupa nyingine zaidi kwa gharama ya shilingi 11,000 (elfu 11) mhimu uwe na miaka 18 kwenda juu.

Jambo lingine la kuzingatia ni kuwa mikao hii (staili hizi) ni kitu kinachoweza kuleta maumivu au majeraha hasa kwa mwanamke kama haitafanyika kwa tahadhari na umakini mkubwa.

Mwanaume asitumie nguvu nyingi au kufanya tendo kwa fujo sana, kama mwanaume amelewa sana ni vema mwanamke ukatae kumpa sukari kwa staili hizi ili kulinda afya yako.

Kama mwanamke hana afya nzuri ya kutosha ni vema asikubali kutumia mikao hii.

Kuna wanawake kwa mfano wana matatizo kwenye viungo vyao na wana matatizo kama ya kusikia maumivu wakati wa tendo la ndoa, kupata michubuko kirahisi na wengine wana tatizo la kuwa na uke mkavu muda mwingi, hawa hawashauriwi kukubali kufanya tendo la ndoa kwa kutumia mitindo hii.

Ikiwa utahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kukusaidia kupata ujauzito niachie ujumbe kwenye WhatsApp +255714800175

Share post hii kwa ajili ya wengine uwapendao.

Imesomwa na watu 48
Style za kupata mimba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *