Vitu vya kuacha unapotafuta ujauzito

Vitu vya kuacha unapotafuta ujauzito

Last Updated on 18/07/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Wakati unatafuta ujauzito chakula au vinywaji unavyotumia vina mchango mkubwa katika kufanikisha wewe upate ujauzito.

Ulivyo ni kile unachokula kila siku. Unahitaji kuwa makini sana miezi mitatu mpaka sita kabla hujapata ujauzito.

Uangalizi pia uendelee hata baada ya kuwa umepata ujauzito.

Vitu vya kuacha unapotafuta ujauzito

Watu wengi niliokutana nao kwa habari ya matatizo ya kutopata ujauzito na nikawashauri juu ya vyakula vya kuacha na kula wengi wao hawachelewi kupata matokeo mazuri.

Kama umekuwa ni mhanga wa kutafuta ujauzito kwa kipindi kirefu bila mafanikio nakuomba uache kutumia vyakula na vinywaji vifuatavyo:

1. ACHA KUVUTA SIGARA

vyakula vinavyozuia kupata ujauzito

Pengine tayari umeanza kupanga kuacha kuvuta sigara utakapopata ujauzito lakini ni vema zaidi kama utaacha tabia hiyo sasa wakati ukitafuta ujauzito na utakuwa umeusaidia mwili kwa kiasi kikubwa sana kuwa na uwezo wa kubeba ujauzito.

Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, wanawake wanaovuta sigara au bidhaa nyingine za tumbaku uwezo wao wa kushika ujauzito ni mdogo ukilinganisha na wale wasiovuta.

Mayai ya mwanamke anayevuta sigara yanakuwa na uwezekano mkubwa wa kupatwa na matatizo yasiyo ya kawaida ya kijenetiki.

Uvutaji sigara kwa mwanamke anayetafuta ujauzito unaongeza uwezekano wa mimba kutoka au kuharibika mara tu upatapo au mimba kutunga nje ya mji wa uzazi (ectopic pregnancy).

Kwa kifupi tabia hii ya uvutaji sigara kwa mwanamke anayetafuta ujauzito inapelekea shida kubwa kwenye mfumo wa uzazi wa mwanmke.

Wakati huo huo siyo wewe tu mwanamke ndiyo unapaswa kuacha kuvuta sigara ikiwa unahangaika kupata ujauzito bali hili linatakiwa lifanyike pia kwa mmeo kwani tafiti zinaonyesha wanaume wanaovuta sigara wanapatwa na tatizo la kuwa na mbegu chache na mbegu kukosa nguvu ya kukimbia kwa kasi na uwezekano mkubwa wa kuwa na mbegu zisizo sawa.

Soma pia hii > Dawa ya asili ya kuzuia mimba kuharibika

2. ACHA VINYWAJI VYENYE KAFFEINA

Relax: Huhitaji kuacha kabisa kikombe chako cha kahawa asubuhi.

Matumizi kidogo ya kahawa kwa siku hayana madhara ya moja kwa moja ya kuzuia usipate ujauzito. Hii inashauriwa usizidishe kikombe kimoja cha kahawa kwa siku.

Hata hivyo kama utaweza kuacha kabisa itakuwa vizuri zaidi.

Vile vile inashauriwa kupunguza matumizi ya vinywaji vyenye kaffeina wakati ukiwa mjamzito kwani kaffeina inaweza kuongeza shinikizo la juu la damu, kuongeza mapigo ya moyo kwako na kwa mtoto aliye tumboni.

Kaffeina inaweza kupelekea kupoteza maji mwilini na kwa kiasi kikubwa inaweza kupelekea mtoto kuwa mtegemezi au teja wa kahawa akiwa mkubwa nk hivyo ni vema ukaacha kunywa kahawa sasa.

Kaffeina inapatikana kwenye chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote, malta, redblue, kwenye chokoleti nyeusi nk

3. PUNGUZA AU ACHA KABISA KUNYWA POMBE

Utanisamehe kwa hii taarifa, hata hivyo itakulazimu kuwasahau kwa muda rafiki zako wa bar kwa muda wakati ukitafuta ujauzito.

Kunywa pombe kupita kiasi au kunywa sana pombe wakati unatafuta ujauzito kuna uhusiano wa moja kwa moja na kuwa na mzunguko wa hedhi usio na mpangilio maalumu, kukosa ute wa uzazi, na kuvurugika kwa homoni za estrogen na progesterone mambo yanayoweza kufanya kushika ujauzito kuwa kibarua kigumu kwako.

Vile vile unaweza usitambuwe ni siku gani hasa ya kushika ujauzito kwani dalili zake hazitajitokeza kama wewe ni mlevi wa pombe kila siku.

Vile vile pombe inashauriwa kupunguzwa au kuachwa kabisa wakati uwapo mjamzito. Unaweza kuwa mjamzito na usijijuwe kama mjamzito ikiwa unakunywa sana pombe kila siku.

Mshauri mmeo pia aache pombe ikiwa mmekuwa mkitafuta ujauzito kwa muda mrefu bila mafanikio sababu upo ushuhuda wa wanaume wanaokunywa sana pombe wakipata matatizo ya kuwa na mbegu zisizo na ubora kwa uzazi.

Unaweza kunywa glasi 1 au 2 tu za mvinyo mwekundu kwa siku na si zaidi ya hapo au aina nyingine ya pombe wakati ukitafuta ujauzito.

Soma pia hii > Dawa ya kurekebisha mzunguko wa hedhi

4. DHIBITI UZITO WAKO WA MWILI

Unafikiri unaweza kuwa una uzito kupita kiasi au una uzito mdogo sana?

Tumia kikotoo cha BMI kufahamu ikiwa una uzito wa kawaida au uliozidi au pungufu kwa kutumia fomula hii ifuatayo.

BMI hupatikana kwa kugawa uzito wako na kipeuo cha pili cha urefu katika mita.

Mfano mimi nina uzito wa kg 80 na urefu wa mita 1.84 ili kupata BMI yangu nazidisha 1.84 mara 1.84 = 3.3856 kisha nagawa na uzito wangu, hivyo kg 80/3.3856 unapata BMI ya 23.62 ambayo ni ya kawaida (normal).

Ikiwa unapata BMI ya 18. 5 au pungufu ya hapo au ukipata BMI kubwa zaidi ya 30 unaweza kuwa unapata matatizo ya mzunguko wa hedhi usio sawa, kukosa kabisa hedhi.

Ukiwa ni mwembamba sana au una uzito mdogo kupita kiasi kuna uwezekano usipate kabisa kuona siku zako na hata mimba isitungwe.

Hivyo ni mhimu kufuatilia uzito wako wa mwili ikiwa umekuwa ukihangaika kwa muda mrefu ukitafuta ujauzito.

Kama hujuwi ikiwa una uzito sahihi na unashindwa kutumia hicho kikokotoo niandikie uzito na urefu wako wa sasa hapo kwenye comment nitakusaidia kukotoa mimi mwenyewe.

Uzito kupita kiasi kwa mwanamke anayetafuta ujauzito unaweza kupelekea matatizo mengine ya uzazi ikiwemo kisukari cha mimba, bawasiri, shinikizo la juu la damu, mimba kutoka, homoni kutokuwa sawa nk

Ikiwa unahisi una uzito mkubwa sana au mdogo sana wasiliana na daktari au nesi wako wa karibu juu ya vyakula, vinywaji na mazoezi unapaswa kuzingatia ili kudhibiti hilo.

Soma pia hii > Jinsi ya kuongeza uume bila dawa

5. ACHA TABIA YA KUWA MTU WA KULA NA KULALA

Unaendelea kuleta visingizio vya kutokufanya mazoezi kila siku?

Acha hiyo tabia mara moja

Utafiti mmoja uliofanywa unaonyesha ukiwa bize kiasi na mazoezi ya viungo kama vile kutembea kwa miguu, kukimbia pole pole, kuendesha baiskeli, kuogelea na kusimama mara kwa mara kunasaidia kuongeza uwezekano wa msongo wa mawazo (stress) kupungua, kuwa na uzito sahihi na kuuongezea nguvu mara 2 zaidi mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula.

Wale wenzangu na mimi wa kula na kulala tu bila mazoezi yoyote wanakuwa na wakati mgumu wa kupata ujauzito tofauti na wale wanaojishughulisha na mazoezi ya mara kwa mara.

Punguza kukaa kwenye kiti masaa mengi kuanzia leo na hili linasaidia pia kukuepusha na saratani ya matiti na kuweka sawa homoni zako.

Zingatia pia nimesema mazoezi kiasi, usizidishe kiwango. Walau mara 3 au nne kwa wiki na yasiwe mazoezi magumu sana.

Soma pia hii > Chakula cha Mwanamke anayetafuta Ujauzito

6. ACHANA NA MSONGO WA MAWAZO (STRESS)

Wakati ukitafuta ujauzito mara nyingi unapata ushauri wa kila namna toka kwa watu wengi unaowafahamu.

Moja ya ushauri utaupata ni kujitahidi kutokuwa na msongo wa mawazo (stress). Huu ni moja ya ushauri wa mhimu sana kuuzingatia ingawa hujuwi ni kwanini unaambiwa hivyo na matokeo yake ni nini kama hutazingatia hilo.

Moja ya sababu kubwa kwanini unaambiwa usiwe na stress wakati unatafuta ujauzito ni kuwa stress inaharibu na kuvuruga mfumo wako wote wa uzazi na kinachovurugwa cha kwanza kabisa ni mfumo wako wa homoni.

Ili kupata ujauzito, homoni ya uzazi ijulikanayo kama ‘progesterone’ ambayo huzalishwa kwenye ovari lazima iwe inafanya kazi vizuri na kwa usawa unaohitajika.

Usawa wa homoni hii ya Progesterone ni wa mhimu kama unataka kupata ujauzito bila vikwazo.

Mwanamke anapokuwa kwenye siku za kupata ujauzito joto la mwili wake huongezeka hasa sehemu yake ya chini kuanzia tumboni.

Wakati huo huo joto linaongezeka pia katika homoni ya uzazi progesterone. Ikiwa joto litashuka katika progesterone inamaana tayari mwanamke ameshaingia kwenye siku zake au ujauzito umetoka.

Mwili unapokuwa umesongwa na mawazo mengi (stress) kwa muda mrefu hutengeneza homoni nyingine iitwayo Cortisol ili kuuwezesha mwili kuhimiri hali hiyo ya mfadhaiko.

Sasa hii homoni Cortisol imeundwa kwa homoni kama zile zile zilizomo kwenye homoni ya uzazi progesterone na wakati mwili unapokumbwa na mawazo mengi homoni hizi zote mbili zinaelekezwa kwenye kuushughurikia huo msongo wako wa mawazo na kama matokeo yake hakuna chochote kinachoelekezwa kushughurika na mambo ya uzazi!

Kwahiyo shida inaanzia hapo.

Na ndiyo maana huwa unasikia watu wanasema unapocheka mara kwa mara siku zako za kuishi zinaongezeka.

Ni kwa sababu unapokuwa na furaha kinga yako ya mwili inaongezeka na mambo mengi maishani mwako utaona yanakunyookea kuliko unapokuwa mtu wa kununa nuna tu kila wakati.

Wanandoa wengi ninaokutana nao kwa shida za uzazi ninaowashauri kwamba wakati wakisubiri kurekebisha athari kwenye afya zao za uzazi wajitahidi kadri iwezekanavyo wasiwe na mawazo mawazo wengi wao wanafanikiwa kupata ujauzito ndani ya muda mfupi.

Kuna mtu anauliza inawezekanaje kuondoa hii hali ya msongo wa mawazo na nina tatizo kama hili miaka kadhaa sipati ujauzito?

Sikia, inawezekana na ni rahisi lakini pia inaweza isiwezekane na ikawa ngumu sana kwako kama utaamua iwe hivyo. Ndiyo mwamuzi wa mwisho ni wewe.

Ndoa siyo kuwa tu na watoto. Yaani kinachofanya ndoa iwepo siyo watoto. Wala dhumuni hasa la kuoana siyo watoto. Wala watoto siyo sababu ya kudumu kwa ndoa.

Na tena naweza kuongeza kuwa hata maisha siyo kuoa au kuolewa tu. Kuoa au kuolewa siyo tiketi ya kwenda mbinguni. Pia kuoa au kuolewa ni jambo la hapa hapa duniani tungali tukiwa hai, mbinguni kuoa au kuolewa haipo (Mathayo 22 : 30).

Dunia tayari ina watu weengi sana na hatuelewi itakuwaje miaka 1000 toka sasa sababu ndani ya miaka 100 tu iliyopita idadi ya watu imeongezeka mara 3 zaidi.

Nchi kama China kwa sasa huruhusiwi kuzaa watoto zaidi ya wawili, ni sheria ya nchi kabisa, huruhusiwi kuwa na watoto zaidi ya wawili.

Heshima na kujaliana ndiyo mambo mawili mhimu zaidi katika ndoa.

Sasa unaanzaje?

Mkabidhi Mungu kila kilicho chako, jikabidhi na wewe mwenyewe kwa Mungu.

Mwambie Mungu mimi nahisi (ndiyo sema nahisi na siyo NINA ..).

Mwambie Mungu nahisi nina tatizo la kutokupata ujauzito, hivyo liangalie hilo na unipe majibu kadri ya mapenzi yako kwangu. Basi halafu acha hilo jambo endelea na maisha mengine.

Relax

Ni mhimu jambo hili la umhimu wa kutokuwa na mawazo wakati unatafuta ujauzito lifahamike kwa wanandoa wote wawili.

Msongo wa mawazo peke yake (stress) unasemwa na wataalamu mbalimbali wa afya kwamba unaweza kukusababishia magonjwa mengine mwilini zaidi ya 50 ikiwemo kuharibu mfumo wa homoni, kushusha kinga ya mwili na mengine mengi bila idadi.

Kwa bahati nzuri kuna namna nzuri za kuondoa tatizo la msongo wa mawazo na hivyo kuujulisha mwili wako kwamba upo tayari kushika ujauzito.

Kuwa bize na kazi, fanya mazoezi ya viungo kila siku, kunywa maji mengi kila siku, usikae mpweke, tumia muda mwingi kusali, shiriki tendo la ndoa mara kwa mara, kula chakula sahihi (hasa vyakula vyenye madini ya magnesium), epuka vilevi, epuka ugomvi mdogo mdogo wa kijinga nk

Kama mmekaa zaidi ya miaka mitano na mnaona hakuna dalili kabisa za kupata mtoto basi nendeni kituo cha watoto yatima ombeni mtoto mmoja mkae naye, mmtunze na kumsomesha kama vile ni wakwenu.

Tuna vituo vingi sana Tanzania vya watoto yatima, unaweza kwenda huko na ukapewa mtoto. Utakuwa umetoa sadaka kwa Mungu na atakubariki kwa ajili hiyo.

Kuna mtu anasema sasa mimi nina mali nyingi kama nakufa atarithi nani kama sina mtoto. Pole sana ndugu. Pole.

Nani amekutuma huku duniani kuja kuandaa mali za watoto wako?.

Hizi mali zote ni za Mungu ulizikuta na utaziacha na ni mali kwa ajili ya watu wote akiwemo na mwanao. Kila mtu akizaliwa Mungu humuwekea vipaji vyake vimfanikishe katika maisha yake.

Sasa inapotokea mtoto anazaliwa tayari ana nyumba, tayari ana gari, tayari ana kampuni, tayari ana hela bank kunamfanya mtoto huyu kuwa zezeta, anakuwa hana akili wala busara. Kunamharibia uwezo wa ubongo wake wa kutumika kwa ajili ya jamii yake inayomzunguka.

Zawadi pekee unaweza kumuandalia mtoto ni kumlipia tu ada ya shule.

Kwahiyo kama una mali na huna mtoto ukifa tupo wajomba zako tutarithi. Na kama unaona shida sana sisi turithi mali zako unaweza kuandika waraka kwamba nikifa mali zangu zipelekwe kituo cha watoto yatima.

Kuna ndugu wengine ndiyo wanaleta misongo ya mawazo kwenye ndoa za watu eti utasikia mbona huyo mkeo hazai? Anakula bure tu?.

Kaa mbali na watu wenye mawazo mgando kama hao wanaosema mbona mkeo hazai. Waambie atazaa wakati ukifika na hatukuoana ili kuzaa.

Mme ndiyo unahitajika kuwa na msimamo usioyumba na ndiyo uongoze maombi kila siku nyumbani na mwambie mkeo tutaishi, tutafurahi hata kama hatupati mtoto na muda ukienda sana tutaenda kituo cha watoto yatima tuchukuwe mtoto wetu tuendelee na mambo yetu mengine.

Uwezo wako wa kubeba ujauzito unaongezeka mara mbili zaidi unapokuwa huna msongo wa mawazo.

Ndoa siyo kuwa na watoto tu.

Relax

Funga mkanda wa kiti chako tuendelee na safari

7. ACHA CHIPSI

Chipsi na vyakula vingine vyote vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi havifai kwa mtu anayetafuta ujauzito. Chakula chochote kinachopikwa kwa staili hii ya kuwa katikati ya mafuta mengi vinaweza kusababisha uvimbe kwenye mji wa uzazi (fibroids) pia kwenye mirija ya mayai (ovarian cyst).

Hivyo chipsi, maandazi, bisi (popcorn) yafaa vikae pembeni kwanza ukitafuta ujauzito.

Vyakula hivi ukiacha kusababisha uzito pia ndiyo sababu ya kutokea kwa ukaidi wa insulini (insulin resistance) na hivyo kuwa sababu ya kisukari na kushuka kwa afya ya uzazi.

Vyakula hivi vinasababisha madhara kwenye mirija yako ya damu na hivyo kuharibu mtiririko wa viinilishe kwenda kwenye viungo vyako vya mfumo wa uzazi.

Wanaume pia wanashauriwa kuacha vyakula vya namna hii kwani vimethibitika kusababisha upungufu wa mbegu na ubora wake kwa ujumla.

Vingine utapaswa kuacha ni pamoja na soda, juisi yoyote ya dukani, vyakula vya kwenye makopo, nyama nyekundu na samaki wenye mercury (nunua samaki wa hapa hapa Tanzania achana na wanaotoka sehemu zingine).

Nikipata mengine zaidi nitazidi kuwaandikia …

Kama unatafuta dawa ya asili ya kupata ujauzito, niachie ujumbe WhatsApp +255714800175

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba Asili. 

Ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE, Ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam.

 

Imesomwa na watu 3,048
Vitu vya kuacha unapotafuta ujauzito

3 thoughts on “Vitu vya kuacha unapotafuta ujauzito

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *