Aina 4 za wanawake ambao hawawezi kuolewa

Last Updated on 17/01/2024 by Tabibu Fadhili Paulo

AINA 4 ZA WANAWAKE AMBAO HAWAWEZI KUOLEWA

Makala hii inaeleza juu ya aina 4 za wanawake ambao hawawezi kuolewa au wanaolewa kwa kuchelewa sana.

Vitu vingi ninavyojadili hapa ni tabia na zinaweza kurekebishika iwapo mhusika atakuwa tayari kubadilika.

Kwenye maisha hakuna kitu kizuri au hakuna silaha kubwa unaweza kupata kama kupata ufahamu na uwezo wa kutambua udhaifu wako.

Watu wengi hawapendi kujipeleleza na kujitafiti wapi wanakosea au wapi wana mapungufu. Wengi wanapenda kuonekana ni wakamilifu na namna au tabia yoyote yakutaka kuwaonyesha udhaifu wao inaweza kukuletea shida wewe uliyeanza kutaka kumuonyesha shida zake.

Watu wengi wanapenda kusifiwa tu na siyo kukosolewa. Hili ni jambo baya sana kama wewe ni mtu unayependa kujirekebisha na kuwa bora zaidi ya ulivyo.

Vile vile nitowe angalizo mapema kwamba haina maana kwamba ukiwa mwanamke ni lazima uolewe, au ili uwe umekamilika kama mwanamke basi lazima uolewe au hata mwanaume siyo lazima uwe umeoa ndiyo uwe umekamilika, HAPANA sina maana hiyo.

Wapo wanawake wengi tu hawajaolewa na wana msaada mkubwa katika familia, katika jamii na kwa taifa kwa ujumla.

Kuolewa ni bahati na kwa bahati mbaya ukweli utabaki pale pale kwamba si wanawake wote watapata nafasi ya kuolewa.

Takwimu zinaonyesha kila watoto 10 wanaozaliwa watoto 7 kati yao ni wa kike!

Kuna mambo mengi unayoweza kufanya na jamii inayokuzunguka ikaona fahari kuwa na wewe hata kama hujaolewa au huna mme.

Jikubali

Kusema hivyo bado siwezi kupinga ukweli pia kwamba wapo wanawake ambao wanalala usiku na mchana wakiomba Mungu waweze kupata wenza wa maisha yao na waanzishe familia kama mme na mke na kuwa na watoto.

Siyo jambo baya kuolewa kwani kwa kawaida hakuna taifa linaweza kuwepo kama watu hawaoani.

Hata hivyo kuna baadhi ya tabia unazoweza kuwa nazo kwa kujuwa au hata bila kujuwa zinazoweza kuwa zinazuia wewe kuolewa au kudumu kwenye ndoa na leo nimeona bora nikuandikie tabia hizo ili kama unaweza kuzifanyia marekebisho unaweza kumpata mwanaume umtakaye na ukadumu kwenye ndoa yako.

Aina 4 za wanawake ambao hawawezi kuolewa

1. Mwanamke mkamilifu

Hapa haina maana kwamba msichana mwenyewe ni mkamilifu, hapana. Huyu ni msichana au ni mwanamke ambaye mawazo yake yote ni kupata na kuolewa na mwanaume wa ndoto zake.

Vigezo vyake vya aina ya mwanaume anayemtaka mara nyingi ni vingi mno kiasi kwamba mwanaume wa sifa hizo anaweza asipatikane.

Mara nyingi mwanamke huyu anaweza kumpata mwanaume mwenye sifa hizo lakini bahati mbaya mwanaume huyo anaweza asimpende huyu mwanamke.

Mwanamke huyu anakuwa na sifa na vigezo kichwani kwake vya aina ya mwanaume anayemtaka. Anataka kuwa na mwanaume mrefu, tajiri, mpole na mzuri sana (Handsome man).

Mwanamke huyu anaweza kuendelea kung’ang’ania vigezo hivi kwa kipindi kirefu sana akimtafuta mwanaume asiye na kasoro na mwenye sifa anazotaka yaani mwanaume mrefu, tajiri, anayejali na mzuri sana kwa umbile.

Tatizo la tabia hii : Shida kubwa ya wanawake wa aina hii ni kuwa wanaishia kulipenda BOKSI (container) badala ya kupenda VILIVYOMO ndani ya boksi (content). Unaishia kupenda vitu vya nje vya mtu badala ya kumpenda yeye kama yeye.

Ushauri: Mpende mwanaume kwa jinsi alivyo na punguza hivyo vigezo walau mpaka nusu yake na mengine yatakaa sawa pole pole mkiendelea kuishi.

Kwa mfano ukipata mwanaume mrefu na siyo tajiri unaweza kuolewa naye, utajiri ni vitu vinavyotafutwa na mtu wa aina yoyote anaweza kuupata wakati wowote bila kujali ni mfupi au ni mbaya usoni.

2. Mwanamke mrembo sana

Mwanamke mrembo sana anapendwa na kila mwanaume.

Kuna mwanamke hawezi kumaliza kukatisha njia hajaitwa au hajatongozwa. Ni mzuri kila mwanaume anayemuona anamtamani na kumtaka.

Mwanamke au msichana wa namna hii ni vigumu kuolewa au kudumu kwenye ndoa.

Mara nyingi wanawake na wasichana wa namna hii hujikuta kwenye mahusiano ambayo si sahihi kwao.

Huu ndiyo ukweli mchungu.

Anaweza kupata mwanaume wa kumuoa kirahisi sana na akaolewa mapema sana katika umri wake lakini itakuwa vigumu kudumu kwenye ndoa kwa sababu ya udhaifu wake wa asili yaani uzuri uliopitiliza aliopewa na Mungu.

Umeona eeehhh?

Wanaume wengi wanaotembea au kuanzisha mahusiano na wanawake wa namna hii hufanya hivyo kwa lengo moja la BURUDANI TU na siyo kingine.

Uzuri wako mwenyewe unaweza kukuponza na ukaishia kutumika kama chombo cha starehe tu na ukashuhudia wenzio wenye sura mbaya au za kawaida wakiolewa na kuwekwa ndani kila siku.

Uzuri wake unamfanya kuwa mgumu kujitunza na kujiheshimu kwa ajili ya mwanaume mmoja. Haya ni matokeo ya kuhitajika na kila mwanaume kila kona kulia, kushoto, katikati kila akigeuka anahitajika.

Tatizo lilivyo hasa : Tatizo kubwa la wanawake na wasichana wa namna hii ni kuwa hakuna mwanaume anayetokea kumpenda mwanamke huyu kwa jinsi alivyo na wanaume wengi huwa na viulizo vingi kichwani wakihofu ikiwa kweli msichana au mwanamke huyu anaweza kuwa mama na kuendesha familia kwa utulivu.

Hili linawasilisha hatari kubwa kwa mwanamke kushindwa kuolewa au kuolewa mapema na kuachika kirahisi au mapema zaidi.

Hakuna mwanaume anaweza kuendeleza mahusiano na wewe akiwa na uhakika kabisa kichwani kwamba wewe ni cha wote au ni chama la wana.

Suluhisho kwa tatizo hili : Kuwa na picha ya mwanaume unayemhitaji kuwa naye maishani.

Una bahati kwamba umezaliwa ni mrembo na uwe na uhakika kuolewa kwako haitakuwa shida ila utapata raha zaidi ukichukuwa hatua nyingine ya pili ya kumheshimu huyo mwanaume mmoja aliyekupa Mungu, kuwa mwaminifu kwake na atakuwa na furaha kwa uamuzi wake wa kukuoa.

Wanaume hawataacha kukutongoza, hawataacha kukuhitaji.

Thamani yako ya kweli itaonekana pale tu utakapokataa kutumia uzuri wako kuishi maisha ya kijinga kwani hakuna mwanaume atakayevumilia ujinga wako sababu tu wewe ni mzuri.

Subutu yako! Utaliwa na kuachwa kila mara kama boga.

3. Msichana kutoka familia tajiri

Msichana au mwanamke ambaye baba yake ni tajiri sana naye anaweza kupata wakati mgumu kuolewa.

Akili yake mara nyingi ipo bize na utajiri wa baba yake. Na mara nyingi anaweza kumchukulia baba yake kama vile ni malaika au mungu wa pili.

Akili yake yote ni baba yake na baba yake ndiye shujaa wake kwakuwa kwenye kuishi kwake hakuna alichowahi kuhitaji akakikosa. Akitaka ada analipiwa ya mwaka mzima tangu januari, akitaka simu ya milioni mbili ananunuliwa.

Na wazazi wengi wenye mali hudhani kuwapenda sana watoto wao ndiyo kuwajali kumbe wanawaharibu bila wao kujuwa.

Hakuna mwanaume anaweza kuwa mbadala wa baba yake au mama yake.

Wasichana wengi wa namna hii huwa wanadhani kila mwanaume anayemhitaji anafanya hivyo kwa sababu ya utajiri alionao baba mkwe (baba wa msichana) na wanakuwa hawapatikani kirahisi mbele ya macho ya wanaume.

Wanaume wengi wanaojitambuwa hawawezi kukubali upumbavu wa namna hii. Yaani hata uwe tajiri vipi mwanaume anabaki kuwa mwanaume.

Chochote kinachoweza kumfanya huyu mwanaume asijione mwanaume na mwenye kauli ya mwisho kitakuzuia usiolewe.

Tatizo lilivyo : Wasichana wengi ambao baba zao ni matajiri huolewa kwa kuchelewa sana au huolewa na mwanaume ambaye siyo sahihi kwao.

Suluhisho la tatizo : Tambua mali za kidunia ni ubatili na upumbavu mtupu.

Hela ni kitu cha mhimu sana hakuna mtu hata mmoja atakayepinga hili bali uelewe kuwa HELA PEKE YAKE SIYO KILA KITU.

Hela, majumba, magari, utajili vyote utaviacha hapa hapa duniani, ulivikuta na utaviacha wala visikupe homa kila mtu anaweza kuwa navyo.

Wanaume wanaweza kuvutiwa na wewe sababu ya uhakika wa kuishi maisha yasiyo ya kimaskini lakini ujuwe kuwa uzuri wako utakuwa ni kitu cha pili watakachokupendea jambo ambalo si sahihi.

Kuwa mpole tu dunia tunapita.

4. Mwanamke shupavu 

Hawa ndiyo wale unawasikia kwenye mitandao wanajiita kina strong woman, wanajiita kina boss lady, mwanamke mpambanaji, single woman na kadharika.

Hawa wana kila dalili za kufanana na wanaume.

Hawa wanaamini wanajiweza wenyewe na hawahitaji kuwa chini ya mwanaume.

Wengi wao wana biashara zao binafsi, ni waajiriwa wa serikali kwenye vitengo mhimu au wanafanya kazi kwenye makampuni makubwa na hawana shida yoyote.

Unaweza kumkuta mwanamke tayari ana nyumba yake, kazi nzuri, gari lake, hela ya kutosha, ni mzuri hata kwa umbile lakini kuolewa inakuwa vigumu.

Mara nyingi wanapenda kuwa wanaharakati, ni waumini wazuri wa kauli mbiu ya haki sawa na usimtegemee mwanaume ndiyo kauli zitokazo kwenye midomo yao mara nyingi.

Kwa bahati mbaya ndoa haipo hivyo.

Hakuna haki sawa kwenye ndoa na haitakaa itokee hivyo leo wala kesho wala kesho kutwa, kwa kifupi sahau hilo kichwani kwako.

Ndoa kama ndoa kwao siyo tatizo, mara nyingi wanabahatika kupata wanaume wazuri. Tatizo ni kazi wanazofanya.

Tatizo lao kubwa : Tatizo lao kubwa hawa wadada ni MUDA. Hawana muda na wanaendesha kila kitu kwenye maisha yao kama vile biashara hata mahusiano wanayachukulia kama vile ni kuendesha biashara au kampuni fulani.

Wanaweza kuajiri mpishi na akaishi hata mwaka mzima bila kuingia jikoni japo kuandaa chai ya mmewe. Yupo bize.

Wanapenda kuwa mabosi kwenye kila kitu na hili ni jambo wanaume wengi hawawezi kuvumilia.

Kadri mwanamke anavyojitahidi kutaka kuwa kama au kufanana kimajukumu na mwanaume ndivyo anavyokuwa anapoteza mvuto kwa wanaume.

Hakuna mwanaume yupo tayari kuishi na mwanaume mwenzake ndani ya nyumba moja.

Wanaume wanapenda wanawake wenye sauti ya chini na wanaoonyesha dalili fulani ya kunyenyekea na kujishusha. Ndiyo asili yao wanaume na huwezi kuibadili.

Suluhisho la tatizo : Endelea kuwa mwanamke bila kujali kazi yako, mali zako na uwezo wako wa kujimudu.

Unapoolewa haina maana huwezi kuishi peke yako au huwezi kujimudu, bali hiyo ndivyo tulivyoumbwa kwamba peke yetu hatujiwezi na mara zote tunahitaji misaada ya wengine hata kama siyo misaada ya hela lakini tumeumbwa kutegemeana.

Kuwa mpole, jishushe, cheka na watu, kuwa mtoto.

Je wewe ni mwanamke na unaishiwa au umepoteza kabisa hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa?

Kama ndiyo jibu la tatizo lako ninalo, ninayo dawa nzuri ya asili ya kukurudishia mudi yako kama zamani na ukaendelea kufurahia maisha yako ya ndoa, tuwasiliane WhatsApp +255714800175

SHARE na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 1,038
Aina 4 za wanawake ambao hawawezi kuolewa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *