Chakula cha mgonjwa wa PID

Last Updated on 18/05/2023 by Tabibu Fadhili Paulo

Chakula cha mgonjwa wa PID

Moja ya ugonjwa mbaya sana na unaowakera sana wanawake ni ugonjwa ujulikanao kama PID au Pelvic Inflammatory Disease.

Ugonjwa huu ni maambukizi (infections) kwenye via vya uzazi vya mwanamke na dalili zake ni pamoja na kutokwa na uchafu ukeni wenye harufu kali na inayokera kama vile shombo ya samaki na kumzuia mwanamke kupata ujauzito kirahisi.

Kwenye makala hii sielezi sana kuhusu ugonjwa bali nitatumia muda mwingi kufafanua juu ya chakula kinachofaa kwa ajili ya mgonjwa wa PID.

Ulivyo ni kile unachokula na kunywa kila siku.

Upo uhusiano wa karibu sana wa afya yako na chakula unachokula.

Ingawa kubadili chakula chako na kula vizuri kama inavyopasa mgonjwa wa PID ale hakuwezi kuleta maajabu ya haraka na kuponya PID moja kwa moja, bado inaweza kukusaidia kupunguza maumivu ya PID na kurahisisha kupona kwako.

Kila mara unapokula chakula ni ama unaongeza kinga na afya yako au unaipunguza kutegemea umekula nini hasa.

Kwa upande wa mgonjwa wa PID msisitizo mkubwa uwe ni vyakula vinavyoongeza na kuimarisha kinga ya mwili, hivi ndivyo vinaweza kumsaidia mgonjwa kupona haraka.

Kama unatumia dawa peke yake bila kuzingatia unakula nini inaweza kukuchelewesha sana kupona PID.

Wakati huo huo ikumbukwe kinga ya mwili siyo chakula peke yake bali ni lazima pia mtu uwe na amani na utulivu wa akili.

Kama unakula vizuri lakini bado una mawazo mawazo mengi (stress), huonyeshi dalili yoyote ya kuridhika na maisha yako na hali yako, basi tambua chakula peke yake hakiwezi kukusaidia kuimarisha Kinga yako ya mwili.

Watu wengi sana miaka ya sasa wanasumbuliwa na roho ya kutoridhika na wengi wanatamani kuwa na mali nyingi na kuishi maisha ya kifahari, kuishi hivi ni namna rahisi sana ya kuharibu kinga yako ya mwili bila kujua.

Umepata chakula, mshukuru Mungu, una kazi ya kuajiriwa au una biashara yoyote na inaenda, mshukuru Mungu, umeamka mzima, mshukuru Mungu.

Wakati huo huo ni mhimu sana kwa mgonjwa kupata usingizi wa kutosha kila siku.

Usingizi mzuri wa kutulia.

Usingizi ni moja ya vitu mhimu sana kwa ajili ya kuimarisha Kinga ya mwili na kuwa na afya bora.

Bila kupata usingizi mzuri na wenye utulivu hata ule nini hata unywe dawa gani bado huwezi kupona PID.

Chakula cha mgonjwa wa PID

Chakula cha mgonjwa wa PID

1. Kula zaidi vyakula vyenye madini ya kalsiamu (calcium) kwa wingi kama maharage na mbegu mbegu zote jamii ya kunde, jibini (cheese), ndizi zilizoiva, almond, ufuta, mbegu za chia (chia seeds), dagaa,

2. Vyakula vinavyoondoa sumu mwilini kama vile mboga nyingi za majani na matunda mbalimbali

3. Pikia vyakula vyako mafuta salama na yenye omega 3 kama vile mafuta ya zeituni, mafuta ya Nazi, mafuta ya mbegu za mlonge, mafuta ya samaki na mafuta ya mbegu za maboga na pia jijengee tabia ya kutafuna mbegu za maboga ujazo wa kiganja chako cha mkono kutwa mara 1.

4. Tumia vidonge vyenye vitamini nyingi kwa pamoja ambavyo hujulikana kama multivitamin.

Kama hupendi kutumia vidonge na unapenda kutumia vitu vya asili zaidi ili kupata vitamini nyingi mbalimbali unaweza kutumia unga wa majani ya mlonge.

5. Kula vyakula vinavyoongeza bakteria wazuri tumboni kama vile mtindi, vitunguu swaumu, chai ya tangawizi, kitunguu maji na uji wa Unga wa ndizi.

6. Kunywa maji kila siku kuanzia lita 2 na yasizidi lita 3.

7. Tumia asali badala ya sukari kwenye chakula au kinywaji chochote kinachohitaji sukari.

Hivyo ni vyakula mhimu na vinatakiwa kuwa kwenye orodha yako ya kwanza ikiwa unasumbuliwa na PID.

Ugali, wali, nyama, tambi, viazi unaweza kula pia lakini kwa kiasi kidogo na mara moja moja.

Usisahau pia mazoezi ya viungo mara kwa mara.

Mazoezi siyo lazima uende gym kunyanyua vyuma, kutembea tembea tu au kukimbia kidogo ni mazoezi tosha.

Usikae ndani wakati wote, tembea tembea pia kwenye jua kila siku.

Pia utatakiwa kuacha vyakula, vinywaji na vitu vifuatavyo kwa muda mpaka pale utakapokuwa umepona.

Usile vyakula vifuatavyo kama unasumbuliwa na PID muda mrefu na hakuna dalili ya kupona ;

1. Chai ya rangi
2. Kahawa
3. Soda yoyote
4. Juisi yoyote ya dukani
5. Kilevi chochote
6. Vyakula vinavyopikwa katikati ya mafuta mengi kama vile chipsi, maandazi nk
7. Vyakula vya kwenye makopo vinavyoandaliwa kiwandani.
8. Keki
9. Biskuti
10. Ice cream
11. Mikate
12. Sukari

Kumbuka vyakula hivi ninavyosema uviache siyo vyakula halamu au vyakula vibaya au havifai, hapana, simaanishi hivyo.

Utakapokuwa tayari umepona unaweza kuendelea kuvitumia kwa raha zako, tunavikataza wakati huu ili kukuongezea nafasi ya kupona haraka na kuimarisha kinga dhidi ya PID.

Kitu kingine cha kuepuka ni kushiriki tendo la ndoa kinyume na maumbile kwani ndiyo njia rahisi zaidi ya kuendeleza ugonjwa wako wa PID.

Ni mhimu wakati wote wa matibabu mama asishiriki tendo la ndoa na mmewe pia apatiwe dawa za kudhibiti bakteria, virusi na maambukizi mbalimbali mwilini.

Naitwa Fadhili Paulo, ni Tabibu wa Tiba asili na ni Mtanzania, ofisi yangu inaitwa TUMAINI HERBAL LIFE ipo Kibugumo Mji Mwema Kigamboni Dar Es Salaam Tanzania.

Ikiwa unahitaji dawa ya asili ya kutibu kabisa na kusahau kuhusu PID niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

Imesomwa na watu 52
Chakula cha mgonjwa wa PID

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *