Last Updated on 17/07/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Dawa ya kupevusha mayai ya uzazi
Kama mwanamke, afya nzuri ya mayai ya uzazi ni mhimu kwa ajili ya kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi na kuwa na uwezo wa kushika ujauzito.
Je ni dawa gani nzuri ya asili kwa ajili ya kuongeza afya ya mayai yako ya uzazi? Makala hii inajadili hilo kwa kina.
Endelea kusoma ….
Pamoja na dawa, bado kutakuwa na mabadiliko utakayotakiwa kuyafanya hasa upande wa vyakula ili kuongeza uwezekano wa tatizo lako kuisha kwa haraka na kwa uhakika na hivyo kuongeza uwezekano wa wewe kupata ujauzito.
Hapo kabla iliaminika kwamba wanawake huzaliwa na mayai yote ya uzazi na kwamba mwili hauendelei kuyazalisha mengine.
Miaka ya karibuni imegundulika katika tafiti mbalimbali kwamba seli ndani ya ovari za mwanamke zinaendelea kuzalisha mayai mengine mapya katika mzunguko wa miaka ya uzazi.
Umri unabaki kitu mhimu sababu ingawa mwili wako unaendelea kuzalisha mayai mapya bado mji wako wa uzazi utaendelea kuwa na mazingira yasiyo rafiki kwa afya bora ya mayai kadri umri wako unavyozidi kuongezeka
Kama umekuwa ukiambiwa uwezekano wako wa kupata ujauzito ni mdogo sababu mayai yako yamezeeka basi hilo lisikutishe sababu bado mwili wako unaendelea kuzalisha mayai mengine mapya kila mara na hivyo bado kuna tumaini kwako.
Ni mhimu kula mlo sahihi na kufanya mabadiliko chanya ya kitabia ili kuvutia upevukaji mzuri wa mayai yako.
Inachukua siku 90 mpaka yai liwe limezalishwa na kuundwa tayari kwa kurutubishwa.
Hii ndiyo sababu hatua zozote utakazochukua kuimarisha afya na kukomaa kwa mayai yako lazima zidumu kwa muda mrefu si chini ya miezi mitatu mpaka uone matokeo chanya na mazuri.
Wakati mayai yako yanajiandaa kwa ajili ya kurutubishwa yanaweza kuathiriwa ubora wake na mambo mengi yanayohusiana na hali ya afya yako ya sasa.
SABABU ZA KUTOPEVUKA KWA MAYAI YA UZAZI:
Mara nyingi mayai kutopevuka husababishwa na mabadiliko katika homoni ya ‘estrogen’.
Mabadiliko haya mara nyingi hutokea wakati wa kuvunja ungo, wakati wa hedhi, wakati wa ujauzito na wakati wa ukomo wa hedhi (menopause).
Vitu vingine vinavyopelekea mayai kutopevuka ni pamoja na
- Kuongezeka umri
- Lishe duni
- Kutokujishughulisha na mazoezi
- Kupungua kwa ogani ya adreno
- Mfadhaiko (stress)
- Kukosa usingizi
- Dawa za uzazi wa mpango
- Sumu na kemikali mbalimbali mwilini nk
VITU HIVI USIVITUMIE ILI KUBORESHA AFYA YAKO YA MAYAI:
1. Vyakula vya viwandani
2. Mafuta yatokanayo na wanyama
3. Soda
4. Kaffeina – chai ya rangi, kahawa
5. Vilevi
6. Sukari
Kama utahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kupevusha mayai ya uzazi bonyeza hapa.
Kama utanunua kutoka kwangu nitakuwa karibu na wewe kila siku mpaka nione umefanikiwa kutibu tatizo lako.
Napatikana live WhatsApp nyakati zote za mchana kila siku.