Je unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako?

je unaweza kupata mimba wakati wa hedhi

Last Updated on 29/06/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Je unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako?

Hili ni moja ya swali kongwe sana kwenye mada zinazohusu uzazi.

Ni swali ambalo linaulizwa sana hasa na wanafunzi au na watu wasio tayari kupata ujauzito.

Swali hili huulizwa pia na watu wazima walio kwenye ndoa ambao wameshatafuta ujauzito kwa muda mrefu bila mafanikio.

Kwenye majibu yangu nitakuwa na majibu yote mawili yaani NDIYO na HAPANA.

Na nitaeleza kwanini NDIYO inawezekana na kwanini HAPANA haiwezekani.

Endelea kusoma …

Je unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako?

a) Ndiyo unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako.

Sababu kuu moja kwanini unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako ;

1 : Anayeleta ujauzito hasa ni Mungu mwenyewe

Ukweli ni kuwa anayeleta ujauzito ni Mungu mwenyewe.

Na Mungu hana mipaka na hapangiwi chochote, anaweza kufanya lolote wakati wowote.

Kwa kawaida ujauzito huja tu wakati wowote.

Na kila mwanamke ni wa pekee na hafanani na mwingine yoyote.

Ndiyo maana wengine wana mizunguko ya siku 21, wengine 22, wengine 28, wengine 32 na kadharika.

Ingekuwa wanawake wote kote duniani wote wana mzunguko wa siku 28 basi ingekuwa ni rahisi sana kufahamu kila mwanamke anaweza kupata ujauzito siku gani.

Kwenye Biblia kuna habari ya mwanamama mmoja anaitwa Sarah ambaye tunasoma yeye alipata ujauzito akiwa na miaka 90.

Kwa akili za kawaida hilo haliwezekani lakini kwa Mungu hilo ni dogo sana.

Ukiona hupati ujauzito na ukaanza kupeleleza ni siku gani utapata ujauzito ujuwe tayari kuna kitu siyo sawa kwenye mwili wako.

Wenye watoto wengi ukikaa nao watakuambia jinsi ambavyo ghafla tu walijikuta ni wajawazito.

Hakuna fomula ya jumla juu ya lini hasa unaweza kupata ujauzito.

Kuna mwingine anapata ujauzito muda mchache kabla ya kuona siku zake, mwingine anapata mara tu baada ya kumaliza siku zake, mwingine anapata ujauzito kuanzia siku ya 11 tangu aanze kuona siku zake, mwingine kuanzia siku ya 14 kabla ya kuona hedhi nyingine na kadharika.

Kwa hiyo linapokuja suala la lini utapata ujauzito ni siri ya Mungu na lolote linaweza kutokea wakati wowote.

Ukiishi na mmeo miezi 6 au mwaka mmoja kitanda kimoja na haupati ujauzito acha kusumbua watu kuuliza uliza eti lini utapata ujauzito, hapo ni wazi kuna kitu si sawa kwenye mwili wako.

Mtu mwenye uwezo wa kupata ujauzito hahitaji kujua wala kuwa bize kupeleleza lini atapata ujauzito.

Ataona tu tayari ni mjamzito.

Mimi nina watoto wanne mpaka sasa na sijawahi kukaa hata siku moja kufikiri leo nitampa ujauzito au leo sitampa.

Wewe endelea kushiriki tendo la ndoa na kama unahitaji kupata ujauzito ondoa hilo wazo kichwani, endelea kushiriki bila kuwaza chochote na siku isiyojulikana utajiona ni mjamzito.

Mara nyingi ukiwa bize sana unawaza kupata ujauzito basi hiyo ni sababu moja wapo kwanini hupati ujauzito.

Usiwaze. Usijipe mawazo BURE. Endelea na maisha yako.

Kuna mtu anauliza sasa kama kupata ujauzito ni mpango wa Mungu mbona yeye hapati na anaomba kila siku?

Sikia ndugu; kila jambo lina wakati wake na maksudi yake chini ya jua.

Mkabidhi Mungu shida yako na uendelee na maisha yako, yeye anajua ni lini hasa ni muda muafaka kwako kuwa na mtoto.

Kumbuka kuna mengi tu mazuri ambayo Mungu amekupa ambayo hata hukuwahi kumuomba.

Soma Mhubiri 3 : 1 – 8

Maisha ni jumla ya mambo mengi na hatupo hapa duniani kwa lengo la kuzaa tu na kuwa na watoto, kuna mengine mengi unaweza kufanya kwa ajili yako, familia yako, ukoo wako, jamii yako na taifa lako ambayo hayana uhusiano au ulazima wa wewe kuzaa.

Wanaounga mkono hoja hii kwamba NDIYO unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako wanashikilia ile dhana kwamba mbegu za kiume zinaweza kubaki ukeni masaa 48 hadi 72 bila kufa hivyo kama mama alikuwa ni wa kupata ujauzito mara tu baada ya kumaliza siku zake basi mbegu hizo zinaweza kumkuta na kumtungisha ujauzito.

Hoja hiyo haina mashiko sana na niseme tu uwezekano wa wewe kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako ni mdogo sana sawa sawa na hakuna.

kupata ujauzito ukiwa kwenye hedhi

.

Ikiwa umekuwa ukitafuta ujauzito kwa muda mrefu bila mafanikio bonyeza HAPA.

Je unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako?

b) HAPANA, Huwezi kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako.

Sababu kuu mbili kwanini huwezi kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako :

2 : Kwa sababu siyo busara kushiriki tendo la ndoa ukiwa kwenye siku zako

Sababu kuu inayonifanya nikatae kwamba huwezi kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako ni kutokana na ukweli kwamba ukiwa kwenye siku zako siyo nyakati sahihi za kushiriki tendo la ndoa.

Kidini na kimaadili kwa ujumla si sahihi kushiriki tendo la ndoa ukiwa kwenye siku zako.

Hata kama ni dharura, siyo sahihi.

Kwanza jambo lenyewe ni la siku 3 au siku 5, limezidi sana ni siku 7, sasa unashindwa vipi kuvumilia siku 7 damu zitoke, ziishe na ubaki msafi?.

Labda kama umekutana na mpenzi wako kwa ghafla na hujaonana naye miaka kadhaa.

Lakini kama ni mme unayeishi naye au hata kama ni mchumba unakutana naye mara kwa mara siyo busara kulazimisha ushiriki tendo la ndoa ukiwa kwenye siku zako.

Kwa hiyo ukiwa kwenye siku zako huwezi kupata ujauzito kwa sababu hizo siyo siku za kushiriki tendo la ndoa.

Ifahamike hakuna madhara ya moja kwa moja ya kiafya anayoweza kuyapata mama au baba endapo watashiriki tendo la ndoa mama akiwa kwenye siku zake, ila tu kimaadili si jambo zuri.

Na tena wapo baadhi ya wanawake wanapokaribia kuona siku zao au hata wanapokuwa wakiendelea kuziona siku zao hushikwa na hamu sana ya kutaka kushiriki tendo la ndoa.

3 : Kwa sababu hakuna yai la kurutubishwa ukiwa kwenye siku zako

Mtu anayeuliza uliza kama anaweza kupata ujauzito akiwa kwenye siku zake au la ni mtu ambaye hajuwi ni nini hasa kinatokea mpaka mwanamke anaona siku zake.

Ni hivi, ile damu unaanza kuiona unapoanza siku zako ni yai ambalo lilikuwa lirutubishwe na mbegu ya kiume ili ujauzito upate kutungwa.

Sasa kwa sababu hilo yai halikurutubishwa, yaani hukupata ujauzito ndiyo hilo yai linapasuka na kunatokea damu ambayo ni damu ya hedhi.

Kama ungekuwa ulipata ujauzito usingeziona hizo siku zako.

Sasa yai tayari limepasuka na tayari unaziona damu, hakuna yai tena mpaka utakapokaribia tena kuona siku zako za hatari siku ya 14 hivi kabla ya hedhi yako nyingine hasa kama una mzunguko usiobadilika wa siku 28.

Kwa hiyo ukiambiwa utapata ujauzito ukiwa kwenye siku zako muulize huyo mtu anayekuambia hivyo ni yai lipi tena litatungishwa huo ujauzito wakati tayari limepasuka na damu unaziona?

Ni matumaini yangu umenielewa vema mpaka hapo.

Ukiwa na swali lolote kuhusu makala hii niulize hapa hapa chini kwenye sanduku la comment na nitakujibu tena hapa hapa BURE.

Ila ikiwa unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175

Share post hii na wengine uwapendao.

Je unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako? Share on X
Imesomwa na watu 2,240
Je unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako?

2 thoughts on “Je unaweza kupata ujauzito ukiwa kwenye siku zako?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *