Last Updated on 23/05/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Kosa kubwa 1 wanalofanya wanaume wengi pale wake zao wanapochelewa kushika ujauzito
Nipende kutumia nafasi hii kutoa pole kwenye ndoa yoyote ambayo wamekuwa wakipitia changamoto ya kutopata mtoto kwa kipindi kirefu.
Ninafahamu ni kwa jinsi gani tatizo hili linavyosumbua kwenye nyumba nyingi hasa miaka ya karibuni.
Nafahamu kabisa kama ningetangaza kwamba natoa bure dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito basi ningekuwa na foleni isiyoisha kila siku.
Wapo waliohangaika mpaka wamekata tamaa.
Wameshatumia pesa nyingi, wameshatumia dawa nyingi lakini bado hakuna majibu.
Wengine wamekuwa ni watu wa mawazo tu muda mwingi na hawana amani kabisa moyoni.
Hakuna furaha kwa mtu yoyote hata kama ni tajiri kama hana mtoto.
Kila mtu yupo bize anahangaika na maisha kwa ajili ya mambo mengi lakini namba moja huwa ni kwa ajili ya watoto wake.
Utamuona baba anaamka mapema saa kumi na moja anaoga na kuelekea kazini au kwenye mihangaiko mingine kwa ajili ya watoto wake.
Thamani ya mtoto haijulikani.
Yaani kungekuwa na namna watu wakawa wanauza watoto na unaenda kununua kama vile tunavyonunua viatu dukani nadhani bei yake hakuna mtu angeweza.
Juzi nilikuwa napitia pitia status za rafiki zangu huko WhatsApp nikaona mmoja amepost viatu nikavipenda.
Nikamuuliza bei akanijibu ni laki 1 na elfu 20.
Hiyo ni gharama ya kununua tu viatu pea moja!
Sasa mtoto angeuzwa bei gani?
Haijulikani.
WhatsApp natumia namba hii +255714800175.
Kuna waliohangaika sana kutafuta mtoto kwa miaka kadhaa na wanaamua kutumia huduma ya kupandikiza mtoto.
Kwa Tanzania huduma hii ya kupandikiza ujauzito inagharimu kati ya milioni 4 mpaka milioni 10.
Lakini wapo walio tayari wanalipa hizo milioni 10 kwa wanaopandikiza ujauzito ili kupata mtoto.
Dar Es Salaam, Arusha na Dodoma huduma hii inapatikana.
Kwahiyo nafahamu ni madhira gani wanapitia wanandoa ambao hawafanikiwi kupata mtoto kwa kipindi kirefu.
Wengine wanaishi na stress, wengine wanatishiana kuachana, wengine wameishiwa hata hamu yenyewe ya tendo la ndoa na wanaweza kukaa hata wiki 3 hawajagusana.
Hali huwa mbaya zaidi mwanamke anapofikisha miaka 35 au 40 na bado hajapata mtoto.
Kwa kifupi tu niseme siyo jambo rahisi kuishi na tatizo hili hasa ukizingatia maneno maneno ya ndugu, jamaa, marafiki na majirani juu yenu.
Sasa kosa kubwa 1 wanalofanya wanaume wengi pale wake zao wanaposhindwa kupata ujauzito ni kuweka majukumu yote kuhusu tatizo hilo kwa wake zao pekee.
Yaani mwanaume anafikiri sababu kubwa ya wao kutopata mtoto ni mwanamke na yeye mwanaume haimhusu.
Jumba bovu lote anaangushiwa mke!
Ni mke ndiyo atapelekwa kufanya vipimo kisha majibu yanasema ni uvimbe kwenye kizazi au homoni zimevurugika au mayai hayapevuki, au ana chango la uzazi na kadharika, orodha haiishi.
Atapatiwa dawa moja baada ya nyingine na hapo mwaka unaweza kupita, miaka miwili hata mitatu hata miaka mitano inaweza kupita bado wapo bize kuhangaika na matatizo ya uzazi kwa mwanamke peke yake!
Hapo mwanaume hana hata wazo la kufanya vipimo kujua ikiwa na yeye huenda ni sehemu ya tatizo.
Na wapo wanaume kabisa ambao hukataa wazi wazi kufanya vipimo hata baada ya daktari kushauri mmeo naye afanye vipimo.
Wanakataa kupima hata baada ya wake zao kuwaomba na wao kupima.
Na baadhi ya wanaume ninao chat nao WhatsApp wana kisingizio cha kwamba wana watoto wa miaka miwili au mitatu au miaka kumi kabla ya kuoana na mke wa sasa.
Mwanaume kama alipata mtoto sehemu nyingine miaka miwili nyuma moja kwa moja anajiona ni mzima na hana tatizo la uzazi.
Hivyo mwenye tatizo atakuwa ni mkewe tu.
Hapo ndipo mnapokosea sana.
Kama ulipata mtoto miaka miwili nyuma au hata miezi 6 nyuma, haina maana hutapata tatizo fulani kwenye mfumo wako wa uzazi linaloweza kuwa ndiyo chanzo cha mkeo wa sasa kutopata ujauzito.
Narudia tena : Kama wewe mwanaume unaye mtoto kabla ya kuoana na huyu mke wa sasa ambaye hapati ujauzito haina maana tatizo lote lipo kwa mwanamke.
Unaweza kutungisha ujauzito mwezi huu na mwezi ujao ukapata tatizo la kuwa na mbegu chache, mbegu zisizokomaa vizuri, wingi wake unaweza kupungua pia na kadharika.
Wakati wowote unaweza kupata tatizo la kushindwa kutungisha ujauzito.
Hata kwa wanawake ipo hivyo kwamba anaweza kupata mtoto wa kwanza, wa pili na wa tatu vizuri tu lakini baadaye ikawa shida kupata ujauzito wa nne mpaka apate dawa ndiyo anapata ujauzito.
Hili mbona unalifahamu lakini unashindwa kulieguza upande wako?
Wanawake wengi wanashikwa na mshangao kuona waume zao hawana habari ya kupima na majukumu yote wanapewa wao.
Nimeshawaona wanawake wenye uvimbe kwenye kizazi au tumboni na bado kwa neema ya Mungu wanapata ujauzito.
Kumbe kwenye familia nyingine ikitokea mama amepima na amekutwa na uvimbe basi jukumu lote anaachiwa yeye.
Mpaka apone uvimbe mke ndiyo wanaamini watapata ujauzito.
Unakuta Mungu anamsaidia huyu dada kweli uvimbe huo anapona lakini bado hawapati ujauzito.
Daktari akimpima anarudisha majibu hana uvimbe na hana tatizo lolote linalozuia asipate ujauzito.
Lakini bado mpaka hapo mme hana habari ya kupima na pengine anahamishia mawazo kwamba huenda ndugu yao fulani anawaloga, kumbe hakuna uchawi wowote zaidi ya uvivu wake au woga wake wa kuchukua vipimo.
Ninaweza kuendelea kuandika na kuandika mengi sana kuhusu jambo hili lakini hoja yangu kuu ni kuwa inapotokea ndani ya nyumba yenu mnashindwa kupata mtoto, mwanaume usiache jukumu lote liwe kwa mwanamke.
Na wewe shiriki vipimo na uwe sehemu ya suluhisho.
Tena uzuri mwingine ni kuwa vipimo kwa wanaume huwa ni bei ndogo sana ukinilinganisha na gharama za vipimo hivyo hivyo kwa mwanamke.
Na ikitokea kuna tatizo fulani kwenye mbegu zako linaloleta shida usitungishe ujauzito niachie tu ujumbe WhatsApp 0714800175 ninayo dawa nzuri sana ya asili kwa ajili kuimarisha mbegu za kiume na hivyo uwe na afya yako tena na kwa njia ya asili bila madhara mengine yoyote mabaya.
Tafadhali mwanaume toa ushirikiano kwa mkeo pale inapotokea mmeishi muda mrefu bila kufanikiwa kupata mtoto.
Pia kwa wale wanandoa wapya au wale mliopo kwenye ndoa changa nawaomba kujifunza kuwa na subira.
Siyo mnaoana leo miezi mitatu tu baadaye tayari mpo bize mmeanza kujiuliza mbona ujauzito hautokei!!
Hamkuoana kwa ajili ya ujauzito tu.
Miezi 6 tu tayari watu wameanza kuuliza dawa ya kupata ujauzito.
Mna haraka ya wapi?
Jaribuni kuishi kwanza hata miaka miwili ya mwanzo bila kuwa na presha yoyote ya kuwa na mtoto.
Na hata muda unapopita sana bila mafanikio bado hamhitaji kuwa na presha yoyote, na presha au stress inaongeza tu tatizo na kulifanya gumu kutibika.
Relax, tulia, omba Mungu, tumia dawa lakini bado endelea kumshukuru Mungu kwa uzima ulionao hadi sasa.
Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao