Last Updated on 14/12/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
Nitajuaje kama ujauzito wangu umetoka?
Kama unatafuta dawa ya asili ya kuzuia ujauzito usitoke wasiliana na mimi kwa kubonyeza hapa
Dalili za wazi kabisa za ujauzito kukutoka ni damu kutoka na maumivu ya tumbo.
Onana na daktari wako wa karibu kwa haraka endapo unahisi ujauzito wako umekutoka.
Wakati mwingine unaweza usione dalili zozote za kutoka ujauzito wako labda mpaka ufanye kipimo cha ultrasound.
Wakati mwingine unaweza kujihisi huna ujauzito wala huonyeshi kuwa na dalili za ujauzito kukutoka.
Hizi ni dalili moja wapo zinazoweza kukutokea ujauzito wako ukikutoka;
- Kutokwa na damu ukeni
- Maumivu makali ya tumbo
- Tumbo kuvurugika
- Presha inaweza kupanda
- Unaweza kuanza kutokwa na uchafu ukeni
Vipo vitu vingine ambavyo vinaweza kukuletea dalili kama hizo hapo juu ambavyo havihusiani na ujauzito kutoka.
Lakini kama unahisi ujauzito unaweza kuwa umekutoka wahi haraka uonane na daktari.
Usijiulize mara mbili mbili wala usianze kutaka kupata majibu kwenye mtandao au kwa watu mitaani, wahi uonane na daktari kwanza kwa usalama wako.
Dalili za ujauzito kutoka zinaweza kuwa tofauti toka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine.
Siyo kila ujauzito unaokutoka lazima ukuletee maumivu.
Maumivu yanaweza kuwa makali kweli kwa baadhi ya wanawake na yakawa ni ya kawaida tu au yasionekane kabisa kwa wengine.
Unaweza kutokewa na maumivu kama yale unayoyaona wakati unakaribia kuingia au ukiwa kwenye siku zako.
Ni kawaida kwa mjamzito kuona damu zikitoka ukeni na wakati mwingine zikiambatana na damu yenye mabonge mabonge wakati mwingine mabonge yenye ukubwa wa limau ndogo wakati ujauzito unapokutoka.
Linaweza kuwa ni jambo gumu na la kushangaza lakini kama limeshatokea huna namna zaidi ya kulipokea na kumwachia Mungu.
Zoezi hilo la damu kukutoka na maumivu yake vinaweza kuisha haraka au vinaweza kuendelea kukutokea kwa masaa kadhaa.
Daktari atakupa dawa na dondoo kadhaa juu ya namna ya kuishi ili kudhibiti maumivu hayo wakati wa kutoka ujauzito wako.
Haijalishi inakutokea kwa haraka kiasi gani au imekutokea mara ngapi, suala la kutokwa na ujauzito ni jambo linaloumiza sana kimwili na kiakili.
Ukiwa mjamzito jitahidi kuwa karibu na daktari wakati wote na uwe na mawasiliano yake ili iwe rahisi yeye kujua nini kinaendelea na ujauzito wako.
Daktari wako atakusaidia kufahamu kujua kipi ni cha kawaida na kipi si cha kawaida na kukupa msaada japo wa mawazo juu ya nini chakula na nini hutakiwi kula ili kuwa salama zaidi.
Ukienda hospitali usichukuwe tu dawa na kuondoka, chukua pia namba ya daktari.
Nini nitegemee kunitokea baada ya ujauzito kunitoka?
Hakuna hali moja ambayo kila mwanamke anajisikia baada ya ujauzito kutoka.
Unaweza kutokewa na hisia au mihemko mchanganyiko ikiwa ni pamoja na kujisikia huzuni, kuchanganyikiwa, unaweza tu ukajisikia vibaya, unaweza kujiona na hatia na kadharika.
Ukiweza kulia lia tu vizuri na hali hizo zitapotea zenyewe kadri muda unavyoenda.
Jitahidi kuwa karibu na kuzungukwa na watu sahihi wenye upendo na msaada kwako ili kukusaidia kipindi hiki kigumu unachopitia.
Tambua kuwa hata mmeo naye atakuwa na huzuni na mawazo ya hapa na pale na atakuwa anaumia kama unavyoumia wewe na pengine hata zaidi ya unavyoumia wewe.
Mnatakiwa kuendelea kuonyesha upendo kwa kila mmoja na kumtanguliza Mungu.
Ni muda gani utachukuwa mpaka maumivu ya kimwili na kiakili kupotea baada ya ujauzito ni tofauti kwa kila mwanamke.
Unaruhusiwa kusikitika na kulia pia lakini isiwe shida kwani ukifanya hivyo kwa muda mrefu hakuna faida yoyote utapata zaidi ya kujiongezea madhara mengine tu ya kiafya.
Ruhusu maisha mengine yaendelee.
Kama utahitaji kupata ujauzito tena utatakiwa kusubiri miezi kadhaa ipite walau miezi 6.
Lakini kama ndiyo mara ya kwanza ujauzito kukutoka unaweza kusubiri kwa miezi mitatu hivi kabla ya kutafuta ujauzito mwingine tena.
Kumbuka usipoupa muda mwili wako wa kusubiri kidogo na kujiripea tena upya na ukakimbilia kudaka ujauzito mwingine kwa haraka huo nao unaweza kukutoka tena.
Ninashauri kabla hujaamua kupata ujauzito mwingine baada ya ujauzito kukutoka utumie dawa ya asili kuzuia ujauzito kutoka miezi miwili kabla ya kupata na mwezi mmoja tena au miwili baada ya kupata ili kulinda usikutoke tena.
Kama utahitaji dawa ya asili ya kuzuia ujauzito usitoke mimi ninayo, wasiliana na mimi ili kuipata dawa hiyo kwa kubonyeza hapa.
Je vipi kama nimekuwa na tatizo la kutokwa na ujauzito mara kwa mara au mfululizo?
Dunia hii ni ya ajabu sana.
Kuna mtu kila akipata ujauzito unamtoka.
Yaani kila akipata ujauzito ndani ya wiki 3 au mwezi mmoja au miezi miwili umemtoka!
Na nimeshakutana na watu wenye tatizo kama hili.
Kama ni hivyo itakulazimu kufanya vipimo zaidi kuona ikiwa kuna tatizo au matatizo mengine maalumu yanayoleta hali hiyo kwako.
Utatakiwa uangalie kama homoni zako, au kama una tatizo lolote la kurithi linalopelekea hali hiyo, au ikiwa kuna viinilishe fulani unakosa mwilini mwako na kwenye mji wako wa uzazi na kadharika.
Hizo ni dalili unazoweza kuziona ikiwa ujauzito wako umekutoka.
Ukiwa na swali zaidi usisite kuuliza hapo chini kwenye comment nami nitakujibu.
Ikiwa unatafuta dawa ya asili ya kupata ujauzito haraka bonyeza tu hapa.
Nitajuaje kama ujauzito wangu umetoka? Share on X