Sababu 4 kwanini hupati ute wako wa uzazi

Last Updated on 17/11/2021 by Tabibu Fadhili Paulo

Sababu 4 kwanini hupati ute wako wa uzazi

Ute wa mimba ni ute unaovutika, ni ute muhimu sana linapokuja suala la kutungwa kwa ujauzito.

Ute huu ambao huvutika mithili ya yai husaidia mbegu kuogelea na kupenya kwenye mlango wa kizazi na kwenda kulirutubisha yai kwenye mirija.

Baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinapelekea kukosa ute wa mimba ili usishike mimba isiyotarajiwa.

Tatizo la kukosa ute wa mimba linachangia pia uchelewe kupata ujauzito. Baadhi ya wanawake watahitaji kutumia kwanza dawa za kuongeza ute ili kushika mimba.

Ute ute laini unaovutika ni wa mhimu ili kuweka mazingira mazuri ya kushika ujauzito.

Siku chache kabla ya mimba kutungwa ute ute laini unaovutika huanza kuzalishwa kwa wingi kwenye mlango wa kizazi.

Katika ulaini wake ute huu unaleta mazingira mazuri kwa mbegu za mwanaume kuogelea kupenya mlango wa kizazi.

Changamoto yoyote kwenye ute maana yake mbegu haitapenya na mimba haitatungwa.

Sababu 4 kwanini hupati ute wako wa uzazi

1. Kama madhara ya matumizi ya baadhi ya dawa

Baadhi ya dawa unazotumia kujitibu maradhi mengine zinaweza kukuletea matatizo kwenye ute wako wa uzazi.

Ute kukauka au kukosa kabisa ute au ute wa uzazi kupungua wingi wake kunaweza kutokea kama matokeo ya dawa zingine unazotumia kujitibu magonjwa mengine.

Baadhi ya dawa zinazotumika kutibu magonjwa yafuatayo zinaweza kuathiri ubora wa ute wako wa uzazi;

*Dawa za kutibu mzio (aleji)
*Dawa zinazotibu au kutuliza kikohozi
*Dawa za kutibu homa na matatizo ya kupumua (hasa kama zinatibu pia kikohozi na aleji)
*Baadhi ya dawa zinazotibu tatizo la kukosa usingizi
*Dawa zinazotibu kifafa
*Dawa za kuondoa msongo wa mawazo

Wakati ni wazi na inajulikana kwamba dawa zinazotibu homa na aleji zinaweza kusababisha kupungua kwa wingi wa ute wa uzazi (kama vile ambavyo zinapunguza msongamano puani kwako), Bado hakuna uthibitisho wa kisayansi wa moja kwa moja kwamba zinaweza kukusababishia ugumba au hali ya wewe kushindwa kupata mtoto.

Kwa kawaida dawa hizo hutumika ndani ya siku chache tu unapoumwa homa au aleji hivyo hupaswi kuziogopa sana.

Kumbuka siyo dawa zote za kutibu magonjwa haya zina madhara ya namna hii kwenye ute wako wa uzazi, zipo ambazo ni rafiki na ni mbadala mzuri kwako.

Ongea na daktari wako wa karibu anayeshughulika na tatizo lako la uzazi kwa karibu na umuombe asikupe dawa za kutibu homa au aleji zinazodhuru au kuingilia afya ya ute wako wa uzazi.

Mweleze pia kwa uwazi kabisa daktari wako uliyemchagua kushughulika na tatizo lako la uzazi juu ya dawa nyingine yoyote unayotumia kutibu chochote ambacho hakihusiani na uzazi.

Pia unao uwezo wa kutumia dawa za asili zisizo na madhara ili kutibu maradhi hayo hapo juu.

Soma hii pia > faida 15 za kushiriki tendo la ndoa mara kwa mara

Angalizo: USIACHE KUTUMIA DAWA AU USIBADILI DAWA YOYOTE UNAYOTUMIA BILA RUHUSA YA DAKTARI WAKO WA KARIBU.

2. Umri

Kadri unavyozidi kuwa na umri mkubwa hasa kuanzia miaka 35 hivi kwenda juu unaweza kuanza kuuona ute wa uzazi kwa siku chache kidogo kidogo tofauti na ulipokuwa msichana.

Ubora na wingi wa ute wako wa uzai pia huanza kupungua kidogo kidogo.

Ukiwa kwenye umri wa miaka 20 hivi hapo mpaka miaka 28 unaweza kuwa unauona ute wa uzazi kwa kipindi cha mpaka siku tano na unapata ute bora na wenye afya.

Kuanzia unapofikisha miaka 30 mpaka miaka 40 na kuendelea mpaka miaka 45 unaweza kuuona ute wako kwa muda usiozidi siku 3 au 2.

Hata hivyo hali na mabadiliko hayo hotofautiana sana toka mwanamke mmoja hadi mwingine.

Hiyo ni fomula tu ya jumla lakini haitokei hivyo kwa wanawake wote. Wapo baadhi ya wanawake wachache mpaka anafikisha miaka 45 bado anaona ute bora na wenye afya na kwa siku mpaka 5.

Kadri unavyokuwa na siku nyingi za kupata ute bora wa au ute sahihi wa uzazi ndivyo na uwezekano wako wa kupata ujauzito unavyokuwa mkubwa.

Kumbuka nimesema uwezekano mkubwa, kwani bado kuna uwezekano wa kupata ujauzito hata kwa yule anayeona ute kwa siku moja tu.

Ndiyo maana huwa napenda kukusisitiza kumtanguliza Mungu na usimwekee sana Mungu mipaka.

Haijalishi ni siku ngapi unazouona ute wako wa uzazi, haijalishi pia ikiwa una miaka 35 au zaidi, ikiwa umekuwa ukihangaika kutafuta ujauzito bila mafanikio ndani ya miezi 6 au mwaka mmoja unapaswa kufanya vipimo na ikiwezekana mfanye vipimo wote wawili wewe na mmeo kubaini ni shida gani ndiyo inasababisha msipate ujauzito.

Ni vipimo pekee, na siyo dalili fulani au ramli ya mganga fulani ndiyo inaweza kutoa jibu la uhakika shida ni nini hasa mpaka hupati ujauzito.

Wengine kwa uvivu huwa wanakimbilia kutaka kujua siku ya wao kupata ujauzito kwamba ndiyo suluhisho la tatizo lao.

Kama afya yako ya uzazi ipo vizuri tu, huhitaji kujua ni siku gani ndiyo ya wewe kupata ujauzito. Utajiona tu tayari ni mjamzito.

3. Matumizi ya Dawa za kupevusha mayai za Clomid

Hii ni dawa ya hospitali ambayo hutumika kwa wanawake wenye matatizo ya uzazi hasa wanaohangaika na kupevuka kwa mayai yao.

Unaweza kushangaa kuona dawa inayotibu tatizo la uzazi ikawa kwenye orodha ya vitu vinavyoweza kuharibu ute wako wa uzazi!

Ikubukwe siyo kila mwanamke anayemeza dawa hii anapata tatizo la kukosa ute.

Jambo hili hutokea tu kwa wanawake wanaotumia dawa hii kwa muda mrefu.

Endapo utagundua uke wako ni mkavu ama unakosa ute wa mimba baada ya kumeza clomid, mjulishe daktari mapema.

Daktari ataweza kukupa dawa zingine mbadala kuondoa madhara haya.

4. Kuwa na uzito pungufu

Homoni ijulikanayo kwa kiingereza kama ‘estrogen’ ndiyo inayohusika na kuongezeka kwa ute wa uzazi unaopelekea kutungwa kwa mimba.

Ikiwa uzito wako upo chini au una uzito pungufu kwa mjibu wa urefu wako na wakati huo huo unafanya sana mazoezi ya viungo kupita kiasi; usawa wa wingi wako wa homoni ya ‘estrogen’ hupungua.

Kupungua huko kwa estrogen hakusababishi kupungua kwa wingi na ubora wa ute wako wa uzazi peke yake, bali pia kunakuletea tatizo la kushindwa kupata ujauzito.

Ikiwa utaongeza uzito na kuacha kufanya sana mazoezi kunaweza kukusaidia kutibu tatizo hili.

Ikiwa utahitaji virutubishi au dawa lishe ili kuongeza uzito wako niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175.

5. Maambukizi kwenye mji wa uzazi

Maambukizi ya bakteria au fangasi kwenye uke hupelekea ukavu na kukosa ute wa mimba.

Fangasi ukeni husababisha dalili za muwasho, kutokwa na uchafu mwingine mweupe na maumivu kwenye tendo.

Harufu mbaya ukeni ni dalili ya maambukizi ya bakteria.

Magonjwa ya zinaa pia yanaweza kupelekea ukose ute wa mimba pamoja na kuziba kwa mirija ya uzazi kama hutatibiwa mapema.

Soma hii pia > Dawa ya asili inayotibu PID

6. Kama homoni zako zimevurugika

Kama homoni zako hazipo sawa na zimevurugika basi hiyo ni moja ya sababu zinazoweza kukuletea shida kwenye ubora na afya ya ute wako wa uzazi.

Na homoni kutokuwa sawa ni kama janga la kitaifa kwa sasa. Wanawake wengi sana miaka ya sasa hili ndilo tatizo linalowasumbua.

Kama huoni ute wako wa uzazi au unaona ute wa uzazi usioeleweka kuna uwezekano mkubwa ni matokeo ya kuvurugika kwa homoni zako.

Ingawa wakati huo huo bado unaweza ukawa na homoni zilizo sawa na unauona ute wa uzazi kabisa kwa wingi na bado ukawa hupati ujauzito (kwa kiingereza tatizo hili hujulikana kama ‘anovulation’) na lina sababu zake za kutokea ambazo nikipata muda nitaandika makala nyingine tofauti kulielezea kiundani.

Ndiyo maana kuna nyakati huwa nakutana na mwanamke ananiambia amefanya vipimo vyote mara kadhaa na homoni zake zipo sawa lakini bado hapati ujauzito.

Ikiwa utahitaji dawa ya asili kwa ajili ya kuweka sawa homoni zako bonyeza hapa.

7. Kusafisha uke kupita kiasi (Douching)

Kuosha uke mara kwa mara hupelekea kuondoa bakteria wazuri wa ukeni na kwenye kizazi na hivyo kuongezeka hatari ya kupata maambukizi na pia kupungua kwa uteute ukeni.

Ni muhimu kuacha kuosha uke mpaka ndani zaidi, badala yake osha mwanzoni tu mwa uke.

Inashauriwa pia uepuke kutumia sabuni na manukato ukeni .

SHARE POST HII NA WENGINE UWAPENDAO

Sababu 4 kwanini hupati ute wako wa uzazi Share on X
Imesomwa na watu 2,757
Sababu 4 kwanini hupati ute wako wa uzazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *