Last Updated on 22/09/2020 by Tabibu Fadhili Paulo
Sababu 9 zinazosababisha ukose au uchelewe kuona siku zako
Kwa mwanamke kuchelewa kupata hedhi huwa hakushitui iwapo mwanamke anajua ni nini tatizo au sababu iliyopelekea yeye kukosa hedhi.
Na majibu ya kuchelewa kwa hedhi hupatikana pindi hedhi hiyo inapochelewa.
Mfano kama ulikua unategemea kupata mimba, ikichelewa inakua ni dalili ya kwanza ya wewe kuanza kufikiria jambo ulilolitaka linaelekea kutimia na hata ukatabasamu na kuwaza hatua nyingine ya kujipima nyumbani au kuenda hospitali.
Na kama hukuwa umetarajia ndio hivyo tena mawazo ya kila aina yatakuja kichwa kutaka kujua kwanini hedhi yako imechelewa na pengine usipate majibu kabisa.
Naitwa Tabibu Fadhili Paulo, mawasiliano yangu ni WhatsApp +255714800175
Sababu 9 zinazosababisha ukose au uchelewe kuona siku zako
1. Umeacha kutumia dawa za uzazi wa mpango
Kama umekuwa ukitumia aina yoyote ya dawa ya uzazi wa mpango za kizungu iwe ni vidonge, sindano, kijiti na kadharika mara tu utakaposimama kuzitumia dawa hizi linaweza kukutokea tatizo la kutoona siku zako.
Dawa hizi za uzazi wa mpango za kizungu kwa sehemu kubwa wakati unazitumia zinaweza kurekebisha mzunguko wako wa hedhi na hivyo unapoacha kuzitumia mwili wako unaweza kupatwa na mshituko.
Hakuna maelezo zaidi ya kwanini mwili wako unapatwa na mshituko huu baada ya wewe kuacha kuzitumia dawa hizi lakini kinachojulikana ni kuwa mwili wako utahitaji muda fulani au miezi kadhaa mpaka urudi kwenye hali yako ya kawaida kama zamani kabla hujaanza kutumia dawa za uzazi wa mpango.
Jambo moja la kuwa nalo makini hapa ni kwamba bado unaweza kupata ujauzito wakati huu hata kama huoni siku zako kama matokeo ya kuvurugika kwa siku zako yaliyotokana na kuacha kutumia dawa za uzazi wa mpango.
Kwa hiyo ikiwa hutaki kupata ujauzito unahitaji kuwa makini sana wakati huu kwani unaweza kupata ujauzito wakati wowote ikiwa utashiriki tendo la ndoa bila kinga.
2. Inawezekana umepata ujauzito
Hata kama umekuwa ukitumia dawa za uzazi wa mpango na umekuwa makini sana katika hilo bado kama unaona hupati siku zako ghafa kuna uwezekano umepata ujauzito.
Hili ndiyo linapaswa kuwa wazo lako la kwanza ikitokea siku zako zimeacha au unaona zinachelewa sana.
Hii inatokana na ukweli kuwa wakati mwingine dalili za mwanzo za ujauzito zinaweza kufanana sana na dalili za kutaka kuona siku zako na inaweza kuwa shida kutofautisha dalili za mimba na dalili za kutaka kuona siku zako.
Kwahiyo kama umekuwa ukishiriki tendo la ndoa mara kwa mara na ghafla unaona huoni tena siku zako ni vizuri kufanya kipimo kuona ikiwa ni mjamzito au la. Fanya kipimo kila baada ya wiki mbili.
3. Umepata ugonjwa fulani
Wakati mwingine ukitokewa ukaona hupati siku zako inaweza kuwa ni matokeo ya wewe kuumwa au kupatwa na ugonjwa fulani mkubwa.
Homa, mafua, aleji au ugonjwa wowote mkubwa unaoweza kuklazimisha kwenda hospitali vinaweza kuwa sababu ya wewe kukosa siku zako kama kawaida.
Magonjwa yanaweza kuwa chanzo cha kuleta mfadhaiko au msongo wa mawazo katika sehemu ya ubongo inayohusika na kuweka sawa homoni na hivyo kuvuruga mzunguko wako wa kawaida.
4. Inawezekana una uvimbe
Je chuchu zako zinatoa maji maji ya maziwa?
Wanawake wengi ukikutana nao wenye matatizo ya uzazi watakuambia wameacha kuona siku zao na wanatokewa na maji maji katika chuchu zao za maziwa na wanapata maumivu ya kichwa ya mara kwa mara.
Ikiwa umepata uvimbe hasa katika tezi ya pituitari (prolactinoma au benign tumor) uvimbe huu unaweza kusababisha kuzalishwa kwa wingi kwa homoni iitwayo prolactin.
Homoni ya prolactin inapozalishwa kwa wingi kuliko inavyohitajika na mwili inaweza kukuletea tatizo la kukosa siku zako sababu inaingiliana kimajukumu na kuzuia homoni ya estrogen kuzalishwa.
Wakati wowote homoni ya estrogen inapokuwa ndogo au chache mwili wako unapata wakati mgumu kuleta hedhi yako na kukufanya usione siku zako.
5. Unafanya SANA mazoezi ya viungo kupita kiasi
Unaenda gym au kufanya mazoezi hata kama unahisi umechoka sana na kazi za kutwa nzima? Au kwa kifupi unaishi kwenye mazoezi?
Kufanya sana mazoezi na huku unakula chakula kidogo na huku unatokewa na kupungua uzito kwa haraka vyote hivi vinaweza kuwa sababu yaw ewe kukosa siku zako hasa kama BMI yako inashuka chini ya 19 au 18.
Unachohitaji hapa ni kupunguza mazoezi na kuongeza uzito kidogo kama ulishuka sana kama matokeo ya mazoezi.
Kumbuka kama inakutokea unakosa kuona siku zako kwa muda mrefu pengine zaidi hata ya mwaka basi ni hatari kwa afya yako hasa afya ya mifupa kama inavyowatokea wamama wengi baada ya siku zako kukoma baada ya miaka 45.
6. Una mfadhaiko wa akili (stress)
Labda unakabiliwa na mzigo mkubwa wa kazi kazini kwako au una shida nyingine tu za kila siku zinazokufanya uwe na mawazo mawazo kila mara inaweza kuwa sababu kwanini huoni siku zako.
Mfadhaiko, msongo wa mawazo, mvurugiko wa akili au stress kwa kiingereza ni kitu ambacho kinaweza kuufanya mwili wako uamuwe sasa siyo wakati wa wewe kupata ujauzito na hivyo kukataa kukupa siku zako.
Mfadhaiko wa akili unaweza kukuletea tatizo la mayai yako kushindwa kupevuka vizuri.
Hii njia ya asili ya mwili ili kukulinda wewe.
Wakati wowote utakapoamua kuachana na stress mwili wako utakurudishia hedhi yako na mzunguko wako utarudi na kutulia kama mwanzo.
Kwanini mwili unapunguza kasi ya upevushaji wa mayai wakati wa msongo wa mawazo?
Mwili unatambua kwamba upo kwenye kipindi cha hatari na unatakiwa upambane ili uishi kutokana na hatari inayokuwa mbele kwa hivo maisha ni kitu cha kwanza ndipo swala na hedhi lifuate.
Mwili utatengeneza homoni za kudhibiti stress kwa wingi kama cotisoli na adrenalini ili kukuandaa kupambana, ama kukimbia hatari iliyopo mbele yako.
Fikiria pale unapotembea usiku na ukaona kitu kisicho cha kawaida mbele yako, tazama mwili unavyobadilika, sasa mabadiliko ya homoni pale unapokutana na kitu cha hatari ni sawa na vile unapopata msongo wa mawazo.
Kadiri mawazo yanavyokuathiri ndivyo uvyonaharibu mpangilio wako wa mwili na kukupelekea ukose hedhi.
Soma hii pia > Kama una stress ni vigumu kupata ujauzito
7. Homoni zako zimevurugika
Hii ndiyo sababu namba moja ya hedhi yako kuacha kutoka au kuvurugika.
Tezi ya thairodi ni kiungo chenye umbo la kipepeo.
Kiungo hiki kipo kwenye shingo chini ya koromeo la sauti.
Kazi kuu ya Tezi hii ni kuzalisha homoni za (T3) na (T4), ambazo kwa pamoja hufanya kazi ya kurekebisha mzunguko wa damu na kazi mbalimbali za mwili.
Matatizo kwenye tezi ya Thairodi kama kushuka kwa uzalishaji wa homoni ama tezi kufanya kazi kupita kiasi huweza kuleta mabadiliko pia kwenye kiwango cha homoni za estrogeni na cotisoli.
Kiwango cha cotisoli kwenye damu kinapokuwa kingi hupunguza uwezo wa tezi ya thairoidi ambapo matokeo yake ni kushuka kwa kazi za mwili kama upevushaji wa mayai na uzalishaji wa homoni za kike
Vile vile lishe mbaya yenye upungufu wa virutubisho ikiwemo vitamini na madini na yenye sukari na viambata vya kuongeza ladha kwa wingi hupelekea tezi za Adrenali na Thairodi kufaya kazi kupita kiasi.
Kitendo hiki hupelekea uzalishaji wa kichocheo cha cotisoli ambacho kinapunguza uzalishaji wa homoni za uzazi.
Cotisoli inapokuwa nyingi zaidi pia inaweza kuleta madhara mwilini kama udhaifu wa mifupa, ngozi kuharibika, tishu za ubongo na misuli kudhoofika na kukupa wewe tatizo la kuvurugika au kukosa hedhi.
8. Umeongezeka uzito
Kama vile ukiwa na uzito pungufu kunaleta tatizo la kukosa siku zako kadharika uzito uliozidi au unene uliozidi pia unaweza kukusababishia ukapoteza kuona siku zako.
Wanawake wenye uzito wa juu au unene uliopitiliza wana uwezekano wa mara mbili zaidi wa kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka tofauti na wenye uzito mzuri wa kawaida.
Mwanamke kuwa na uzito uliozidi unaweza kuwa sababu ya matatizo ya homoni zake na uzito kupita kiasi una uhusiano na tatizo linguine la uzazi kwa wanwake lijuliknalo kwa kitaalamu kama Polycystic Ovarian Sydrome (PCOS).
Kama unataka kupungua uzito wako kwa njia salama bonyeza hapa.
9. Umepata watu wengine wa kulala nao chumba kimoja
Hili linaweza lisiwe na uthibitisho wa kisayansi lakini tafiti mbalimbali zinasema ikiwa ulikuwa unalala peke yako kwa kipindi kirefu na mara ukapata wasichana wengine wa kulala na wewe chumba kimoja hili linaweza kusababisha kuanza kupata hedhi isiyoeleweka.
Hili ni rahisi kutokea hasa kama umetoka nyumbani na umehamia shule ya bweni au hosteli kitendo hiki cha kuanza kuwa pamoja na wengine na kuzoeana nao kinaweza kukuletea kuvurugika kwa siku zako kama sehemu ya kuzoeana na makundi ya watu wengine.
Wasichana wengi wa chuo wanaweza kukuambia hili limewahi kuwatokea kwenye maisha yao.
Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:
- Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.
- Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.
- CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.
- Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid
- Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
- Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.
How I can return my period
Kuna uwezekano wa kubeba mimba cku ya 9?
Kuhusu siku ya kushika ujauzito jifunze mwenyewe kwa kubonyeza hapa