Last Updated on 08/03/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Sababu kuu 2 za wanawake kupenda kujichua
Nitumie nafasi hii kutoa salamu kwa wanawake wote katika sikukuu hii yao ya leo, siku ya wanawake duniani tarehe 8 machi 2022.
Mimi mpaka hapa nilipo nimefika kwanza kwa kuzaliwa na mwanamke lakini siyo hivyo tu bali nimeshasaidiwa mengi sana na wanawake kwa mengi wakiwemo wanawake ndugu zangu, marafiki zangu na wengine wengi.
Hakuna mwanaume bila mwanamke pia hakuna mwanamke bila mwanaume.
Tunategemeana.
Heri ya Sikukuu ya wanawake duniani 8, March 2022.
Sababu kuu 2 kwanini wanawake wanajichua ;
Watu wengi tunafahamu kwamba kati ya mwanaume na mwanamke ni mwanamke ndiye anayeweza kukaa muda mrefu bila kushiriki tendo la ndoa na bado asipate shida yoyote kubwa.
Ndiyo, mwanamke anao uwezo wa kuishi muda mrefu bila kuhitaji mwanaume.
Kutokana na hilo wanaume wengi huwa wanafikiri huenda wanawake hawajihusishi na vitendo vya kujichua au kupiga punyeto.
Lakini ukweli ni kuwa wanawake nao wanajichua na wanapatwa na madhara yatokanayo na punyeto ingawa madhara yao siyo ya kuonekana kirahisi na wazi kama ilivyo kwa wanaume.
Pia kutokana na mabadiliko ya kijamii na kuingia kwa mtandao wa intaneti wanawake nao wamekuwa wakijihusisha na tabia nyingine mbaya ya kuangalia picha za wakubwa jambo linalowapelekea kuwa watumwa wa kujichua.
Ndiyo, hata mimi zamani nilikuwa nadhani wanawake hawapendi kuangalia picha za X na kumbe sikuwa sahihi.
Wanawake wengi tu nao wanapenda kuangalia picha hizo.
Na kile unaweza kushangaa ni kuwa tofauti na wanaume, wanawake wengi hata wakiwa tayari ndani ya ndoa bado wanaendelea kujichua mara kwa mara.
Zipo sababu nyingine nyingi zinazopelekea wanawake kujichua, zipo nyingi na wao wanaweza kukueleza zaidi ukiwadadisi lakini leo sababu 2 tu kati ya hizo nyingi na siku nyingine nikipata muda nitaandika zaidi sababu hizo.
Sababu kuu 2 za wanawake kupenda kujichua ;
1. Wanajichua ili kuondoa msongo wa mawazo (stress)
Kujichua ni kama ulevi na ukiendekeza zaidi kunaweza kumpelekea mwanamke naye kuwa mraibu (teja) wa ulevi huu.
Kujichua kunawasaidia wanawake wanaojihusisha na mchezo huu kuondoa au kupunguza msongo wa mawazo yaani stress.
Kwahiyo ili kupunguza mawazo kwa muda, wanawake hujikuta wanatumbukia kwenye mchezo wa kujichua.
Wakati mwanamke anajichua na kufika kileleni homoni ya kujisikia vizuri na kuondoa maumivu ‘endorphin’ huzalishwa mwilini na hivyo kumsaidia kujisikia vizuri na mtulivu jambo linalomsaidia kuondoa msongo wa mawazo (stress).
Kama ilivyo kwa wanaume, ni kweli jambo hilo linaweza kukusaidia kuondoa mawazo na ukapata kujisikia vizuri.
Ni kweli unaweza kufanikiwa kupunguza mawazo kwa muda lakini bado jambo hilo lina madhara mengine mabaya kwa afya yako kama utaliendekeza jambo hilo mara nyingi na kwa kipindi kirefu.
Kwahiyo kama ulikuwa unajiuliza kwanini wanawake wanajichua basi moja ya sababu yao ni hii ya kuwasaidia kuondoa msongo wa mawazo.
2. Kujichua kunawasaidia kupata usingizi kirahisi zaidi
Ndiyo, wapo wanawake wanaopata tabu kupata usingizi kirahisi na kwa njia ya asili.
Kila mtu anafahamu umhimu wa usingizi kwa afya ya mwili na akili kwa ujumla.
Hakuna mtu anapenda kukosa usingizi kwa sababu yoyote ile.
Kila mtu anapenda akifika tu kitandani basi mara moja apate usingizi haraka, usingizi mzuri, mtulivu na mororo.
Kuna madhara mengi ya kiafya ya kukosa usingizi au kutopata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala.
Ni jambo la kawaida kabisa hata kama ni mchana au ni asubuhi kwa kawaida mwanamke mara baada ya kumaliza tendo la ndoa na akawa amefikishwa kileleni vizuri kweli kweli basi mara baada ya hapo utamuona analala kidogo.
Ni kawaida na wanaume wote wanajua mara tu baada ya kumaliza tendo la ndoa usiku lazima mwanamke alale usingizi mzito hasa kama amefikishwa kileleni vizuri.
Kwa sababu hii, wapo wanawake wanaojikuta ni wateja wa kujichua kama matokeo ya kukosa usingizi.
Kama ulikuwa hujuwi kwanini wanawake nao wanajichua basi moja ya sababu nyingine ya tatizo hili kwao ni hili hitaji la usingizi.
Kwahiyo kama mwanamke kabla ya kuolewa alikuwa akifikishwa kileleni na anajua kufika kileleni kukoje halafu ikatokea akaolewa na mwanaume ambaye ni dhaifu kitandani au hajuwi namna ya kumfikisha mke kileleni basi mwanamke huyo lazima ataendelea kujichua hata kama tayari ameolewa.
Unapenda kufahamu nini madhara ya kujichua kwa wanawake? Kama ndiyo bonyeza hapa.
Share post hii na wengine uwapendao