Last Updated on 19/08/2022 by Tabibu Fadhili Paulo
Shida na matatizo ya kuzaa watoto mapacha
Hakuna mtu asiyependa kubahatika siku moja apate watoto mapacha.
Hakuna asiyetamani hilo.
Lakini ni wangapi kati yenu huwa mnakaa na kutathmini ni gharama kiasi gani inaweza kuwapata endapo kweli mtabahatika kupata hao mapacha?.
Watu wengi hawafahamu ni nini hasa wanakitaka kwenye maisha yao na hata wale wanaofahamu nini wanataka ni wachache sana wanaofahamu gharama halisi za yale wanayoyataka.
Ukweli ni kwamba kupata ujauzito, kulea ujauzito na kulea mtoto ni gharama kubwa sana.
Kama huamini uliza watu wengine karibu yako watakuambia.
Ndiyo sababu baadhi ya wanawake wakipata ujauzito huchukua maamuzi magumu ama kuutoa huo ujauzito au kuzaa na kwenda kumtupa mtoto.
Siyo kazi rahisi kulea mtoto mpaka afikie umri wa kujitegemea.
Sasa, unapotafuta ujauzito kwanza fahamu unachotafuta siyo kitu cha kawaida, siyo kitu kidogo na gharama zake haziwezi kuwa sawa na kununua mbuzi au ng’ombe.
Unatafuta mtoto, unafahamu thamani ya mtoto? au upo bize tu kutaka na wewe uonekane una kitambi uwe mama K mtarajiwa pasipo kujiandaa kwa lolote?.
Ndugu yangu asikuambie mtu kuzaa ni gharama sana hasa nyakati za sasa na hasa kwa watu wale wanaoishi mijini.
Sasa kabla hujataka kupata hao mapacha leo nimeona nikuandikie baadhi ya gharama utakazoingia mara tu ya wewe kudaka ujauzito wa watoto mapacha.
Lengo langu siyo kukutisha au kukukatisha tamaa, bali ni kukuandaa ili usije kukurupuka na maamuzi yako.
Na mwisho wa siku pamoja na shida hizi zote, faida ya kuwa na watoto ni kubwa sana kuliko shida yoyote unayoweza kukutana nayo wakati wa ujauzito, wakati wa kuzaa na hata wakati wote wa malezi.
Bado mtoto ni mtoto na thamani yake haiwezi kulinganishwa na chochote.
Ukipata muda soma na hii > Vyakula 7 vinavyoongeza uwezekano wa kupata watoto mapacha
Shida na matatizo ya kuzaa watoto mapacha
1. Ujauzito wenye shida nyingi
Wakati mama anapokuwa mjamzito huwa kuna shida za hapa na pale zinazoletwa na ujauzito alionao tumboni.
Shida hizo ni nyingi na zinaweza kuwa ni mama kuumwa mara kwa mara hasa nyakati za asubuhi, kujisikia vibaya ghafla tu, kutapika, kuchagua vyakula, kuongezeka uzito, kupata magonjwa kama vile bawasiri, kisukari, kifafa cha mimba na kadharika.
Hii ndiyo sababu wamama walioajiriwa wakishapata ujauzito huwa wanapewa nafasi ya kupumzika (martenity leave) hadi hapo watakapojifungua na kulea mtoto kwa miezi kadhaa ndipo huwa wanaruhusiwa kurejea tena kwenye kazi zao.
Shida nyingine inaweza kuwa ni mawazo mawazo ya hapa na pale kama vile kuwaza ikiwa ujauzito utabaki salama kwa kipindi chote cha miezi 9, pia wazazi watarajiwa huwa wanawaza ikiwa mama K atakuja kujifungua salama bila kuhitaji upasuaji wala kusababisha kifo kwa mama au kwa mtoto.
Sasa, mama anapopata bahati ya kubeba ujauzito wa mapacha shida zote nilizozieleza hapo juu huwa mara mbili yake kwa sababu ni ujauzito wa watoto wawili watarajiwa.
Kwahiyo shida na matatizo ya kuzaa watoto mapacha huanza mapema mara tu mama anapobeba ujauzito na wakati wote wa kulea ujauzito hata kabla watoto hawajazaliwa.
2. Kukosekana kwa usingizi
Wale wote wenye watoto tayari wanafahamu kuwa usingizi huwa ni shida sana siku za mwanzo mwanzo mara tu mtoto akishazaliwa.
Kuna mtoto akizaliwa tu basi mwezi ule wa kwanza au miezi miwili ya mwanzo tangu azaliwe anaweza kuwa analala mchana tu na usiku muda mwingi yupo macho!
Imeshanitokea hali hii kwa baadhi ya watoto wangu mimi mwenyewe.
Yaani inaweza kufika mahali unaanza kujuta kwanini tumezaa sasa sababu kama baba muda mwingi asubuhi mpaka jioni unakuwa bize na kazi kutafuta mkate wa watoto na ustawi wa familia yako lakini cha ajabu usiku tena badala ya kulala upumzike unakaa kucheza na mtoto ambaye haijulikani atalala saa ngapi au saa ngapi katika huo usiku anaweza kuamka na kukatisha usingizi wenu.
Kama wewe ni mzazi tayari unalifahamu hili ninaloliongelea hapa na kama bado hujawahi kuwa mzazi basi usiwe na wasiwasi siku ukipata mtoto ufahamu kuna kukatishiwa usingizi wakati wowote usiku sababu ya mtoto mchanga.
Sasa, mama anapojifungua watoto mapacha shida hii inaweza kuwa mara mbili yake.
Ukiwa na mapacha kuna uwezekano mkubwa sana usiku mzima ukapita hamjapata usingizi hata kidogo.
Anaweza kuanza kuamka mtoto mmoja akaanza kulia, mkambembeleza kwa muda fulani akatulia na kulala, sasa ile analala tu na pacha wake naye anaamka na kuanza kulia, kwahiyo mnabembeleza huyu na anapoacha tu mwingine tena analianzisha.
Basi, wazazi mkiamka asubuhi tayari mna uchovu wa kutosha na bado mwanaume unahitajika kwenda kazini kuendelea na majukumu yako.
3. Baba naye anahitajika wakati wote wa malezi
Tofauti na mama anapojifungua mtoto mmoja ambapo anaweza kulea mwenyewe muda mwingi bila uwepo wa baba, hali huwa tofauti mama anapojifungua mapacha.
Mama anapojifungua watoto mapacha baba naye anahitajika kuwepo nyumbani muda mrefu kushiriki kulea watoto.
Kama baba nyakati za jioni baada ya kazi alikuwa anapata nafasi ya kupita bar apate bia mbili au tatu, au huwa anapitia kijiweni kwa rafiki zake kupiga stori za hapa na pale ili kusogeza muda kabla ya kurudi nyumbani, anaweza asipate nafasi hizo tena.
Kuna baadhi ya kampuni au baadhi ya sehemu za kazi mama anapojifungua mapacha huwa wanatoa mapumziko kwa wazazi wote wawili kabisa hadi mwanaume ili akae karibu na mkewe wakati wa miezi ya mwanzo baada ya watoto kuzaliwa.
Kwa sababu hii kama mlikuwa mnaishi maisha ya kutoka nje kila siku ndipo mle basi kwa hakika hali yenu ya kiuchumi inaweza kuyumba kidogo kama matokeo ya baba naye kulazimika kuwa sehemu ya kulea kama matokeo ya mama kujifungua mapacha.
4. Gharama za kulea huwa mara 2
Ni kweli tunapenda kubahatika kupata watoto mapacha lakini ukisimuliwa gharama zake hasa za kuwalea kwenye miezi ya mwanzo unaweza kukatishwa tamaa na gharama zao.
Utatakiwa kuwabadilisha nguo watoto wawili kwa wakati mmoja, wakianza kutambaa na kutembea utatakiwa uwe na mikono minne na miguu minne ili kuwaweza.
Ukinunua nguo utatakiwa ununue za wawili na ambazo zinafanana.
Kwa vyovyote vile itakavyokuwa bado utalazimika tu kuajiri dada wa kazi au kuita ndugu yako mmoja aje kuishi kwako ili kukusaidia kulea hasa nyakati za mchana.
Ukinunua baiskeli ya mtoto utatakiwa ununue baikeli 2 kwa pamoja.
Haya yote yanafanya gharama za kulea watoto mapacha kuwa juu zaidi tofauti na kulea mtoto mmoja.
5. Ugomvi wa mara kwa mara baina ya pacha hao
Watu wengi hudhani sababu watu ni mapacha basi watakuwa wanapendana tu wakati wote!
Hata kama watoto ni mapacha na wanafanana kwa kila kitu pengine hadi jinsia bado huwa wana kawaida ya kugombana hapa na pale.
Kwahiyo kuanzia utotoni wakiwa wadogo kabisa itakuwa ni kazi ya wazazi kuwasuluhisha wawili hao wanapogombana na hata kupigana.
Wanapoanza kuwa wakubwa kidogo na kuanza kujitambua kila mtoto anaweza kuanza kutaka aonekane yeye ndiye mwenye haki zaidi ya kuwa karibu na mzazi kuliko mwenzake.
Hali hii inaweza isitokee mama anapozaa mtoto mmoja mmoja kwa kipindi kirefu labda baada ya miaka mitatu au mitano kwani mtoto mwingine anapozaliwa anamkuta mwenzake tayari ni mkubwa kidogo na anajitambua tayari tofauti na kama wangezaliwa mapacha.
Shida zinazoletwa na kuzaa watoto mapacha ni nyingi na siwezi kuzieleza zote lakini wazazi waliowahi kuapata mapacha wanazifahamu shida hizo na unaweza kuwauliza zaidi ili kujiandaa na wewe pale utakapobahatika kupata ujauzito wa mapacha.
Na baadhi ya shida hizo haziishii utotoni tu wakati wa kuwalea, shida zingine huwa zinajitokeza hata wanapokuwa tayari watu wazima kwa mfano wazazi wanaweza kuanza kulazimika kuwapeleka shule au chuo kimoja wote wawili, kulazimika kuwa na marafiki wa aina moja kwa wote wawili, kulazimika kuwataka wawe na kazi moja inayofanana na kadharika na kadharika.
Kwa wewe mwenye ndoto ya kuja kazaa mapacha ni vema ukayaelewa haya mapema ili ujiandae.
Ikiwa upo bize kweli kweli na una shauku ya kupata ujauzito wa watoto mapacha na unahitaji dawa ya asili ya kukusaidia hilo, niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175, dawa hii ya kukusaidia upate watoto mapacha inagharimu 210,000/= (laki 2 na elfu 10) kwa sasa na inaweza kupanda zaidi siku za mbeleni.
Share post hii na wengine uwapendao.
Shida na matatizo ya kuzaa watoto mapacha Share on X