Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

Last Updated on 14/10/2022 by Tabibu Fadhili Paulo

Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

Tumia kikokotoo (calculator) hiki hapa chini kufahamu siku zako za hatari, andika tarehe ya siku ya kwanza ulipoona hedhi yako ya mwisho na ujaze mzunguko wako una siku ngapi kisha bonyeza TUMA na usubiri majibu.

Tafuta siku zako za hatari

Siku ya kwanza uliopoona hedhi ya mwisho

Mzunguko wako ni wa siku ngapi

Ili kufahamu vizuri ni siku zipi ni hatari kwa mwanamke kupata mimba, unahitaji kwanza kujifunza jinsi mzunguko wa hedhi unavyofanya kazi.

Kwa wastani, mzunguko wa hedhi huwa ni siku 28.

Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa siku ya kwanza wakati mwanamke anaanza kuona siku zake na tunaiita ni siku ya Kwanza.

Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

Mzunguko wa hedhi wa kawaida huwa una sifa madhubuti zifuatazo:

1. Idadi ya siku katika mzunguko mmoja

Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida ni siku 21 hadi 35 na ni hapo ndipo tunapata wastani wa siku kuwa 28 yaani [(21+35)÷2].

Hivyo mpendwa msomaji wangu usikariri kuwa mzunguko wa kila mwanamke ni siku 28.

Wapo wanawake wana mzunguko wa siku 27, wengine 25, wengine 35, wengine 29.

2. Sifa ya pili ni uwiano wa idadi ya siku za mzunguko kati ya mzunguko mmoja na mwingine

Hili nalo ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la tendo la ndoa kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatari kwa mwanamke kubeba ujauzito.

Ili tuhitimishe kwamba mwanamke ana mizunguko ya hedhi iliyo sawa, idadi ya siku za mizunguko ya hedhi haitakiwi itofautiane kwa zaidi ya siku 7.

Mfano, kama mwezi wa kwanza uliona siku zako baada ya siku 28, mwezi wa pili ukaona baada ya siku 30, mwezi wa tatu ukaona baada ya siku 35 na mwezi wa nne ukaona baada ya siku 21, bado mzunguko wako uko kwenye uwiano mzuri kwa kuwa mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.

Hivyo usikariri kwamba siku za mzunguko wa hedhi kwa kila mwanamke ni siku 28, hilo halipo. Hizi siku 28 ni wastani tu.

Wengine wanaona siku zao kila baada ya siku 21, wengine kila baada ya siku 25, wengine 29, wengine 35 na bado tunasema mizunguko yao bado ni mizunguko ya kawaida.

Pia fahamu ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyo huyo.

Mfano usitarajie kuwa kama mwezi wa tatu (march) ameona siku zake baada ya siku 28 na mwezi wa nne (april) pia ataona siku zake baada ya siku 28. Si lazima itokee hivyo lakini pia huwa inaweza kutokea.

Mfano, mwanamke mmoja mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28, mzunguko unaofuata baada ya siku 27, mzunguko mwingine baada ya siku 30, mzunguko mwingine baada ya siku 29, mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa kwakuwa tofauti si zaidi ya siku 7 kama nilivyoeleza pale juu.

Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

3. Idadi ya siku za kuona siku zake

Usichanganye kati ya siku za hedhi na mzunguko wa hedhi kwani hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.

Siku ya kwanza ya kuona siku zako ndiyo siku tunaanza kuhesabu mzunguko wako wa hedhi na siyo siku ya kumaliza kuona siku zako kama wengi wanavyodhani.

Kawaida idadi ya siku za siku zako ni kati ya siku 3 mpaka 7. Kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo. Mwingine anaenda siku 3 amemaliza, mwingine siku 4, mwingine 5 mwingine 6 mpaka 7.

Chochote zaidi ya siku 7 si cha kawaida na unahitaji kuonana na daktari kwa uchunguzi zaidi.

4. Wingi wa damu

Hii ni Sifa ya mwisho ya mzunguko wa hedhi na inaangalia kiasi cha damu inayotoka wakati wa hedhi. Hapa kuna wanawake wa aina mbili ambapo mwanamke anaweza kutoa damu ya kawaida na mwingine akatoa damu nyingi sana.

ANGALIA MCHORO UFUATAO:

.

Soma hii pia > Mimba huanza kuonekana baada ya siku ngapi

TUANGALIE KIDOGO JINSI MAYAI YANAVYOKOMAA NA KISHA KUTOLEWA KWENYE OVARI.

Fahamu kuwa mzunguko wa ovari ndiyo huleta mabadiliko katika mfuko wa uzazi.

Kwa kawaida mzunguko wa ovari una hatua kuu tatu zifuatazo;

1. Follicukar Phase

Sehemu hii ya mzunguko huanza siku ya kwanza ya mwanamke kuona siku zake mpaka yai linapokuwa limekomaa

Mayai ya mwanamke huanza kutengenezwa tangu akiwa tumboni mwa mama yake.

Mpaka kufikia umri wa kuvunja ungo, mwanamke huwa na wastani wa mayai yapatayo 400,000 ndani ya ovari. Mayai haya huwa katika hatua ya uchanga.

2. Ovulation Phase

Katika hatua hii ya mzunguko wa ovari, yai lililokomaa hutoka kwenye ovari na kuingia kwenye mirija ya mayai.

3. Luteal Phase

Hii ni sehemu ya mzunguko wa ovari ambao wenyewe huanza baada ya yai kutoka na kuishia kabla ya kuanza kuona siku zake yaani mwanzo wa mzunguko mwingine.

Sasa tutaitambuaje siku ya yai kutoka?

Kiuhalisia ni ngumu kujua siku halisi yai lilipotolewa lakini tunaweza kuzitambua siku nyeti ambazo zitatupa nafasi kubwa ya kutokulikosa yai ndani ya siku hizo.

Fuatilia hapo chini.

ZINGATIA HAPA: Idadi ya siku kati ya mzunguko wa yai na mzunguko wa hedhi ni sawa (Mfano, 28, 30, 35, 25).

Idadi ya siku katika luteal phase ni sawa kwa mizunguko yote na ni siku 14.

.

Soma hii pia > Dawa ya asili ya kupata mimba haraka

ANGALIA HESABU HII RAHISI

Folicular phase +luteal phase =Idadi ya siku katika mzunguko.

Lakini tayari tumeshajua luteal phase haibadiliki, [ni siku 14 katika kila mzunguko]. ovulation phase hapo iondoe maana siku ya kushika ujauzito hutokea masaa machache tu.

Sasa ili kuipata siku ya kushika ujauzito, tunachukua idadi ya siku katika mzunguko mmoja – idadi ya siku katika luteal phase, ambayo haibadiliki [14 days].

Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28, kuipata siku ya kushika ujauzito tunachukua 28-14 tunapata 14, kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipoanza kuona siku zake ni siku ya 14 ndipo yai linakuwa tayari kurutubishwa.

Kwa mwenye mzunguko wa siku 30, tunachukua 30-14 (luteal phase) =16, kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30, siku ya kushika ujauzito inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14 (kuwa makini hapo).

Yule mwenye mzunguko wa siku 35, ovulation day ni 35-14 = 21, kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35, siku ya kushika ujauzito ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.

Sasa baada ya kuijua siku ya kushika ujauzito lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya siku ya kushika ujauzito kwani nazo ni siku hatari pia.

KWANINI?

Mbegu ya kiume inauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 tangu mbegu zimwagwe na yai lina uwezo wa kuwa hai hadi masaa 24 tangu lilipotoka kwenye ovari.

Kwaiyo kama mwanaume akijamiiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovari, mbegu inaweza kuwa hai bado na kutungisha mimba endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo kwa mfano kama siku ya kushika ujauzito ya mwanamke ni siku ya 14, mwanamke akijamiiana na mwanaume siku ya 12, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa.

Kadhalika kama mwanamke ametoa yai siku ya 14 kisha akajamiiana ndani ya masaa 24 mbele, pia anaweza kupata mimba kwasababu kipindi mbegu zinamwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.

Kwa ufupi,ni siku tatu tu ndizo hatarishi sana kwa mwanamke kupata mimba,yaani, siku mbili kabla ya siku ya kushika ujauzito na ndani ya masaa 24 baada ya siku ya kushika ujauzito

Kwa kuongeza, kipindi cha siku za kushika ujauzito mwanamke anapata hamu zaidi ya kushiriki tendo la ndoa kwa sababu ni kipindi ambacho kuna homoni fulani ambazo huchochea hamu hii.

Pia kipindi hiki cha siku za kushika ujauzito joto la mwili la mwanamke hupanda, anajihisi mwili kuchemka tofauti kidogo na ilivyo kawaida yake.

Sasa, kwa vile nimesema kuwa hatuwezi kuwa na uhakika kwa asilimia 100 wa siku ya kushika mimba, basi tunalazimika kutumia kanuni ya kuepuka tendo la ndoa kwa muda wa wiki nzima.

Ambazo ni siku zilizo karibu sana na siku ya kushika mimba kwa wale wanaotumia njia ya kalenda.

Mfano, kama una mzunguko wa siku 30, kuipata siku ya kupata ujauzito chukua 30- 14=16, kwa hiyo siku yako ni ya 16 tangia ulipoanza kuona damu siku ya kwanza. Sasa kama ni siku ya 16, ondoa siku nne kabla ya hiyo siku ya siku ya kushika ujauzito .

Kwahiyo kuanzia siku ya 12 hapo, usishiriki tendo la ndoa.

Pia jumlisha siku 3 mbele, ambapo mwanamke atatakiwa kuanza tendo la ndoa kuanzia siku ya 19 huko ili kuepuka mimba.

Ni matumaini yangu umenielewa mpaka hapo.

Kama utahitaji dawa za asili kwa ajili ya kupata ujauzito bonyeza hapa 

Mjulishe rafiki yako kwenye Twitter naye asome makala hii kwa kubonyeza maneno yafuatayo;

Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba Share on X

Tafadhali SHARE post hii na wengine uwapendao

Imesomwa na watu 42,851
Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

32 thoughts on “Siku ya hatari kwa mwanamke kushika mimba

  1. kuna uwezekano wa mwanamke kupata mimba siku 3 za mwisho kuelekea hedhi? kipind ambapo yai liko tayar kutoka..??

  2. asanteh kwa somo lako lakini tunahitaji hesabu kidogo ili kufahamu njia bora za uzazi wa mpango bila kutumia madawa na vipandikizi
    Endelea kutoa elimu bora zaidi ASANTEH

  3. Nimeisoma kwa makini sana makala yako na kimsingi nimekuelewa. Je ni wakati upi sahihi naweza kupata mtoto wa kike?

      1. Habari .. napenda kujuwa siku za hatar kwa mke wng maana mzunguko wake unanichanganya na sijui mzunguko wa siku ngap maana unabadikarika hv

        16/1/2022- bleed

        16/2/2022- bleed(Siku 32)

        16/3/2022-bleed(siku 29)

        16/4/2022-bleed(Siku 32)

        19/5/2022-bleed *
        Na anakiwe kwenye period damu zinakata siku 7

        Cjajuwa mzunguko wa siku ngap na tr ngap mwez ujao ndo tr zake za hatar

        If God wish I would like to be a father pls help me 2 know

      1. Ndiyo ute wa ovulation ndiyo ute wa kutungia mimba kwa kiswahili. Ovulation ni kiingereza. Hata hivyo unaweza kuuona huo ute na bado usipate ujauzito

  4. Asante doctor na je kama umeanza period tarehe 3/2 ukashiriki tendo tarehe 21/2 kuna uwezekano wa kupata ujauzito

    1. Asante Sana kwa makala yako,je Kuna uwezekano wa kupata mimba ukijamiiana siku nne au tano kabla ya kuingia period?

      1. Mungu akiamua anaweza kukupa ujauzito siku yoyote. Usiwe bize kutafuta ujauzito siku za hatari tu. Pia usiwe na mawazo mawazo yoyote wala presha yoyote.

  5. Je kwa mwanamke ambaye mzunguko wake ni siku 35 ila haueleweki na hujaamiana akiwa katika siku zake za hatari ila bado hanasi mimba shida ni nini???

  6. upo vizuri sana tovuti yako imejikamilisha kwa makala za kuelimisha zaidi kuliko kuhitaji fedha zaidi mungu akubariki

        1. Ndiyo kuna uwezekano huo. Pia usiwe bize na siku za hatari tu, tafuta ujauzito hata katika siku ambazo siyo za hatari kwani mwisho wa siku ujauzito ni zawadi toka kwa Mungu

  7. Naomba unisaidie mwezi may nimeingia period tarehe 16 na mwezi june 13 na mwezi July tarehe 13 the mzunguko wangu wa ngu ni 28 au 30 na ipi tarehe ya ovulation naomba nisaidie

  8. Habari doctor bleed ya mwisho ilikua tar 6 mpk 10 July na akashiriki tendo tar 2 August mpaka leo hajableed…Je,kuna uwezekano wa kupata ujauzito?

  9. Asante kwa SoMo zuri, naomba kuuliza mm nikiwa kwenye siku za hatari Ute unatoka kidogo xana he kunauwezekano was kushika mimba?

    1. Kwanza kabisa hakuna neno xana kwenye lugha ya kiswahili, bali tunalo neno SANA. Hatuna herufi x kwenye kiswahili. Kama umekuwa ukitafuta ujauzito kwa muda mrefu na hupati hatua ya kwanza ni kufanya vipimo kuona tatizo ni nini hasa.

  10. Je mwanamke kaingia leo asubuhi
    mida ya sambil kwenyy siku zake .mkasex mida ya sa nne anaweza pata mimba na ni siku yake ya kwanz kwenye hedhi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *