Last Updated on 25/05/2021 by Tabibu Fadhili Paulo
UKOSEFU WA USINGIZI UNAWEZA KULETA UGUMBA
KITENDO cha kukosa usingizi mara kwa mara wakati wa kulala kuna weza kuonekana ni jambo ambalo halina madhara kiafya, lakini ukweli ni kwamba unapokosa usingizi, hasa kwa muda mrefu, kuna athari kubwa katika afya yako yote, hata kama unakula na kufanya mazoezi vizuri.
Madhara ya ukosefu wa usingizi huathiri mfumo mzima wa mwili, mathalani, mbali ya kuathiri kinga ya mwili na kuongeza hatari ya kupatwa na magonjwa ya saratani, ukosefu wa usingizi huweza kusababisha madhara mengine ikiwemo ugumba au tatizo la kushindwa kushika ujauzito
Kuna orodha ndefu ya tabia ambazo tunafahamu zinaweza kuathiri afya ya uzazi kwa watu wa jinsia zote mbili yaani kwa mwanaume na mwanamke.
Tabia hizi ni pamoja na kuwa na uzito mkubwa, uvutaji sigara na msongo wa mawazo (stress) na sasa unaweza kuongeza tatizo la kukosa usingizi kwenye orodha hii.
Tatizo la kukosa usingizi linasemwa sasa ni moja ya sababu zinazoweza kukusababishia kukosa ujauzito kwa watu wa jinsia zote mbili.
Kuna idadi kubwa ya watu wanaosumbuliwa na tatizo la kukosa usingizi.
Homoni zile zile zinazohusika na usingizi ndizo hizo hizo zinazohusika na masuala ya afya ya uzazi.
Sehemu ya ubongo inayodhibiti homoni zinazohusiana na usingizi katika jinsia zote mbili ndiyo sehemu hiyo hiyo inahusika na uamshaji wa homoni zinazohusika na uzazi kwa wanawake na uzalishwaji wa mbegu na kukomaa kwa mbegu kwa wanaume.
Kwa wanawake kitendo cha kukosa usingizi kwa kipindi kirefu kinaweza kuwa na madhara ya moja kwa moja kwenye homoni kadhaa zinazohusiana na uzazi, homoni hizo ni pamoja na homoni ya estrogen, progesterone, prolactin, luteinizing hormone (LH), na follicle-stimulating hormone.
Kwa mfano kuzalishwa kwa homoni iitwayo luteinizing hormone (LH) kunaweza kuleta usumbufu kwenye uzazi kwani hii hii homoni ndiyo inahusika na kuweka sawa mzunguko wa hedhi na uzalishwaji wa mayai ya uzazi.
Mzunguko wa hedhi usio sawa au usioeleweka unaweza kuleta shida au kuchelewesha uwezo wa mwanamke kushika ujauzito.
Kwa wanaume kuna homoni iitwayo ‘testosterone’ ambayo ni homoni mhimu sana katika uzalishaji wa mbegu za mwanaume zenye afya.
Homoni hii huzalishwa kila siku kawaida wakati mwanaume anapokuwa usingizini na hasa katika usingizi mzito usingizi wa kati ya saa nane na saa kumi na mbili asubuhi. Ubora wa homoni hii mhimu kwa uzazi kwa mwanaume unategemea na kiasi na muda wa usingizi anaopata mwanaume kila siku.
Homoni hii hii pia inahusika na suala la nguvu za kiume kwa wanaume na utaona wazi kuwa mwanaume asiyepata usingizi wa kutosha kila siku ni vigumu pia kwake kuwa na nguvu za kutosha za kiume.
Hili la usingizi lina pande zote mbili.
Tafiti nyingi zimeangalia ukosefu wa usingizi au kutopata usingizi mzuri na wa kutosha kunavyosababisha afya mbovu ya uzazi kwa watu wa jinsia zote mbili lakini hitimisho ni kuwa hata kwa wale wanaopata usingizi mzuri na mwingi lakini wa kupitiliza au wa masaa mengi zaidi ya kawaida nao wanakabiliwa na tatizo hili la kutokupata ujauzito au kuwa na afya mbovu kwa ajili ya uzazi.
Kwahiyo kama inakutokea unalala sana au masaa mengi zaidi ya inavyotakiwa na wewe utakuwa na wakati mgumu wa kupata ujauzito sawa na yule anayepata usingizi kwa shida au anakosa usingizi mzuri na wa kutosha.
Usingizi unahesabiwa kama ni usingizi mfupi au usiotosha ikiwa unapata usingizi chini ya masaa 6. Usingizi unahesabika kama ni usingizi uliozidi kama unapata usingizi unaozidi masaa 9.
Kwa wanaume inashauriwa apate usingizi wa kati ya masaa 7 mpaka 8 au 9 kila siku kwa afya nzuri kabisa ya uzazi.
Utafiti mmoja uliofanywa nchini Taiwan kwa kipindi cha miaka kumi uliohusisha wanawake zaidi ya 16000 ulionyesha kuwa wanawake wenye matatizo ya kupata usingizi wa kutosha na mzuri kila siku walikuwa na zaidi ya asilimia 3.7 ya uwezekano wa kutopata ujauzito ukilinganisha na wale wanawake wengine wanaopata usingizi mzuri wa kawaida kila siku.
Tatizo ni kubwa zaidi kwa wanawake wa umri wa kati ya miaka 26 mpaka 30.
Ukosefu wa usingizi au kupata usingizi usio na utulivu ni jambo ambalo limekuwa likihusishwa na ugumba kwa wanawake na linahusishwa na matatizo mengine ya kiafya kama vile uzito kupita kiasi, kisukari na afya mbovu ya moyo.
Magonjwa haya yanatajwa pia kuathiri afya ya uzazi kwa wanawake.
Wanawake ambao hawapati usingizi wa kutosha wanapata pia tatizo la kuwa na mzunguko wa hedhi usioeleweka, matatizo ya homoni, msongo wa mawazo na hamaki au presha na hivi vyote vinaweza kuwa na matokeo hasi kwa afya ya uzazi.
Sisemi hapa moja kwa moja kwamba kurekebisha tu hali ya usingizi kunaweza kukuletea ujauzito haraka bali ninachokuambia ni kuwa kitendo hicho cha kurekebisha hali yako ya usingizi kutoka kuwa mbaya hadi kuwa nzuri kinaweza kuwa na matokeo mazuri sana kwa afya yako ya uzazi na afya yako ya mwili kwa ujumla.
Maarifa haya ni mhimu sana kwa mtu yeyote ambaye amekuwa akihangaika kupata ujauzito.
Kuna tabia nyingi unazoweza kuzirekebisha kwenye safari yako ya kupata ujauzito ambazo ni pamoja na uvutaji sigara, kiasi cha mazoezi unachofanya, uwezo wako wa kudhibiti msongo wa mawazo na ubora wa usingizi unaopata kila siku.
Pengine utahitaji kuonana na Tabibu ana kwa ana ili akusaidie namna nzuri ya kuzidhibiti tabia hizo hapo juu.
Wakati huo huo unaposubiri kuonana na Tabibu ana kwa ana kwa msaada zaidi unaweza kufanya yafuatayo ili kuboresha afya yako ya usingizi:
• Toka nje na ufanye mazoezi ya viungo kila siku
• Kuwa na muda mmoja wa kwenda kulala na kuamka kila siku
• Zima taa za chumbani, simu, Televisheni na kompyuta
• Pumzika (Relax) kabla ya kwenda kulala, usiangalie kipindi au majibizano yoyote yanayoweza kuudhi au kulipa bili muda mchache kabla ya kwenda kulala
• Usinywe soda au juisi yoyote ya dukani au pombe walau masaa matano kabla ya kwenda kulala
• Kula ndizi zilizoiva 2 au 3 muda mchache kabla ya kwenda kulala
• Epuka ugomvi usio na maana
• Epuka msongo wa mawazo kwa gharama yoyote
Ikiwa unatafuta dawa ya asili kwa ajili ya kupata ujauzito niachie tu ujumbe WhatsApp +255714800175
Tafadhali SHARE post hii kwa ajili ya wengine uwapendao
It’s amazing for me to have a web page, which is useful in favor of my experience.
thanks admin